Home Mchanganyiko TBL Plc yaunga mkono jitihada za Serikali kupambana na COVID-19 kwa kuzalisha...

TBL Plc yaunga mkono jitihada za Serikali kupambana na COVID-19 kwa kuzalisha vitakasa mikono

0

…………………………………………………..

Vitagawiwa bure kwenye vituo vya afya na kwa wananchi

Katika kuunga mkoni jitihada za Serikali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19, Kampuni ya bia Tanzana (TBL Plc) kwa kushirikiana na kampuni ya Diversey East and Central Africa Limited, imeanza kuzalisha vitakasa mikono kwa kutuma malighafi zenye kilevi.

Mkurugenzi Mkuu wa TBL Plc, Philip Redman, amesema kampuni yake itatoa msaada wa lita 681 za vitakasa mikono zikiwa kwenye vifungashio vya lita 5 kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa ajili ya kutumiwa kwenye vituo vya afya nchini pote.

Redman, aliongeza kusema kulinda afya na usalama kwa wafanyakazi wa TBL Plc na familia zao nchini kote, wateja wake na jamii nzima kwa ujumla ni suala ambalo kampuni inalipa umuhimu mkubwa. Alishukuru ushirikiano iliopata kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Wizara ya Viwanda na Biashara na kampuni ya Diversey kwa kufanikisha mchakato huu wa kuzalisha bidhaa za vitakasa mikono kwa lengo la kuunga mkono  jitihada za serikali katika kupambana na ugonjwa wa COVID- 19.

Mbali na kuzalisha vitakasa mikono kwa ajili ya vituo vya afya nchini, TBL itazalisha lita 6,180 katika vifungashio vya mililita 500 kwa ajili ya kuwagawia wateja wake na kwenye jamii sehemu mbalimbali nchini. Vitakasa mikono hivyo ambavyo vimetengenezwa kwa malighafi yenye kilevi ya Ethanol, maji na glycerin vitagawiwa bure sio kwa ajili yake biashara na vina viwango vinavyokubalika na maelezo kuhusiana na matumizi yake.

TBL ina historia ndefu ya kusaidia kukuza uchumi wa kijamii nchini Tanzania kupitia sekta ya kilimo, usafirishaji na viwanda.