Home Mchanganyiko HUAWEI YATOA MCHANGO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUPAMBANA NA UGONJWA...

HUAWEI YATOA MCHANGO KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI ZA KUPAMBANA NA UGONJWA WA CORONA

0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amepokea mchango wa  vifaa vya kuendeshea mikutano kwa njia ya video ambavyo ni cloudlink camera tatu, Cloudlink Mic tatu, Cloudlink TV terminal tatu, Cloudlink Platform pamoja na Thermal Imaging Temperature Measuring System sita vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 940 Kutoka campani ya TEHAMA ya HUAWEI,kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID-19. Pichani, Waziri Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Zhou Xu (wa tano kulia), Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Wu tao  (kushoto) na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, George Mwakyembe. Wa nne kulia  ni Waziri wa Madini, Doto Biteko, wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)