Home Mchanganyiko NIDA ILALA YASEMA IMEPELEKA VITAMBULISHO VINGI SERIKALI ZA MITAA.

NIDA ILALA YASEMA IMEPELEKA VITAMBULISHO VINGI SERIKALI ZA MITAA.

0

Kaimu Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Ilala Bi Zulfa Mnyika akimuonyesha Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati wa NIDA Bw. Geofrey Tengeneza baadhi ya vitambulisho ambavyo vilivyopokelewa katika ofisi hiyo kutoka kituo cha kuzalisha vitambulisho kilichoko Kibaha.

Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma ya usajili kwa ajili ya vitambulisho vya Taifa katika moja ya ofisi za usajili za wilaya.

****************************

Na. Hadija Maloya

Idadi kubwa ya Vitambulisho vya Taifa vilivyopokelewa katika ofisi ya Usajili ya Wilaya ya Ilala kutoka katika kituo cha Uzalishaji vitambulisho cha NIDA kilichoko Kibaha Mkoani Pwani katika kipindi cha kuanzia mwaka 2012 hadi 2019, vimeshapelekwa katika ofisi mbalimbali za Serikali za Mitaa katika Wilaya ya Ilala ili kuwapatia wahusika na vingine vimechukuliwa na wananchi wenye.

 

Kwa mujibu wa Kaimu Msajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Wilaya ya Ilala Bi Zulfa Ally Mnyika vitambulisho ambavyo bado havijachukuliwa na wenyewe ni vichache na waaendelea kuja kuvichukua japokuwa kasi kuvichukua
si kubwa sana.

 

Bi Zulfa alisema awali walikuwa wanawasisitizia watu kuja mwenyewe kwenye Ofisi ya NIDA kuchukua vitambulisho vyao, lakini hivi sasa vikishapokelewa vinatawanya kwenye ofisi za Serikali ya Mitaa kisha kuwatumia ujumbe kwa njia ya simu ili waende Ofisi za Serikali ya Mtaa kuchukua Vitambulisho hivyo, huku wakielezwa kuvifuata wenyewe ofisi ya NIDA Ilala.

 

Amesema hii inafanyika ili kuwarahisishia wananchi kupata vitambulisho vyao huko huko waliko katika vijiji
na mitaa yao, isipokuwa wachache ambao huvifuata ofisini NIDA.

 

“Vitambulisho vichache vilivyopo hapa ni vile vya wananchi waliojisajili kupitia BRELA, kundi la Watunishi wa Umma, Wanachuo na Majeshi kuanzia. Niwaombe wahusika waje kuvichua hapa Ofisi ya NIDA iliyopo Mombasa Ilala” Alisema.

 

Akizungumzia zoezi la usajili Kaimu Msajili huyo wa NIDA Wilaya ya Ilala amesema zoezi hilo linaendelea vizuri na kwamba Kasi ya watu kuja ofisini kwa ajili ya zoezi la Usajili kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa, kwani wanapokea kuanzia watu Sabini hadi themanini tu kwa siku ikilinganishwa na hapo awali ambapo kwa siku walikuwa wanapokea kuanzia watu Mia tano hadi Mia nane.

 

Amesema moja ya sababu ya kasi kupungua ni tatizo la virusi vya corona ambavyo vimeripotiwa kuingia nchini na uwepo wa watu waliopata maambukizi.