Home Mchanganyiko SHULE YA SEKONDARI PONDEANI YAKABIDHIWA KOMPYUTA

SHULE YA SEKONDARI PONDEANI YAKABIDHIWA KOMPYUTA

0

**************************

Mfuko wa Mawasiliano  kwa wote (UCSAF) imekabidhi Shule ya Sekondari ya Pondeani seti ya kompyuta tano (5) na Printa moja (1) kwa ajili ya shughuli mbalimbali za uendeshaji wa shule hiyo.

 

Vifaa hivyo viilivyokabidhiwa hivi karibuni na mdau wa elimu kutoka mkoa wa Kusini Pemba wilaya ya Chake Chake, Bi. Mariam Khamis, ambapo pamoja na mambo mengine amewausiha uongozi wa shule hiyo kuzitumia
seti hizo kwa uweledi na uangalifu ili ziwe chachu katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

“Nawakabidhi vifaa hivi ili mkavitumie kwa malengo na kimkakati wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu” amesema Bi. Mariam.

 

Bi. Mariam amesema kuwa vifaa  hivyo zitakuwa mwanzo mzuri wa shule hiyo kufanya kazi kisasa zaidi na kuongeza uwezo wa shule katika kufanya kazi kiuweledi.

 

Kwa upande wake Afisa Mdhamni kutoka Wizara ya Elimu ya wilayani humo Bw. Mohd Nassor ameishukuru UCSAF kwa kuwakumbuka katika shule hiyo kwani inaonesha ambavyo elimu inatakiwa itolewe sambambana
mabadiliko ya teknolojia ya TEHAMA.

 

“Nimepokea vifaa hivi na kwa niaba ya Wizara ya Elimu tunashukuru kwa utoaji huu kwani kutoa si utajiri bali ni moyo na huu ni mtazamo wa kiuzalendo” amesema Bw. Nassor.

 

Amesisitiza kuwa kompyuta hizo zitakwenda  kufanya mabadiliko ya kiutendaji kazi kwa walimu wa shule hiyo na kuleta ari mpya ya ufundishaji, uaandaji wa mitihani ya wanafunzi na uhifadhi wa  taarifa muhimu za shule.