Meneja
wa hotel hiyo Joseph Ngonyo akizungumza na waandishi wa habari leo
kuhusu kufungwa kwa hoteli hiyo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali
kuzuia mikusanyiko
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort
Muonekano wa Hoteli Tanga Beach Resort
ya uongozi wa hoteli yenye hadhi ya nyota tano ya Tanga Beach resort
iliyoko jiji Tanga imelazimika kufunga hotel hiyo ili kuunga mkono
jitihada za serikali za kuzuia mikusanyiko ili kujikinga na ugonjwa wa
virusi vya Corona vinavyotokisa dunia kwa sasa.
Akitoa tamko
hilo mbele ya waandishi wa habari Meneja wa hotel hiyo Joseph Ngonyo
alisema kuwa wameamua kufunga kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo hapa
Tanzania pamoja na na kudhibiti mkusanyiko wa watu
Alisemam kuwa
awali tayari biashara ya hotel ilianza kususasua kutokana na uwepo wa
ugonjwa huo hivyo kulazima kufunga ili kuzuia mkusanyiko wa waty hasa
katika kipindi hiki cha kuelekea katika msimu wa sikukuu.
“Dunia
sasa hivi na hata nchini kwetu kumekuwa na tatizo la gonjwa la Corona
hivyo tumeamua kusitisha huduma ili kuunga mkono kauli ya serikali ya
kuzui mkusanyiko wa wau wengi pamoja hivyo ili kuwathibiti tumelazimika
kufunga hotel hiyo”alisema Ngonyo.
Aidha aliwataka wananchi
kuacha dhana potofu ambazo zimeanza kusambaa katika mitandao ya kijamii
na kwamba wameamua kuunga mkono juhudi za serikali hivyo shughuli za
hotel zinatarajiwa kuanza tena mwishoni mwa mwezi Mei.
Kwa
upande wake mmoja wa wafanyakazi katika hotel hiyo Hadija Ramadhani
alisema kuwa wamelazimika kuunga mkono maagizo ya serikali ili kupunguza
maambukizi kwa wafanyakazi pamoja na wananchi ambao wanaweza kufika
katika hotel kwa ajili ya kupata huduma.
“Tunaomba watu waachane
na habari za mitandao kwani zinatuchafua lakini lengo letu ni
kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu pamoja na wateja ambao wanakuja
kupata huduma katika hotel yety”alisema Ramadhani
Naye kwa
upande wake mfanyakazi wa Hoteli hiyo kitengo cha mapokezi Khadija
Mcharo alisema kwa sasa huduma zao wamesitisha kutokana na uwepo wa
virusi vya Corona na wanaiunga mkono serikali katika juhudi zake za
kupambana kupunguza maambukizi hayo.