………………………………………………………………………….
Klabu ya Manchester City, kupitia ukurasa wake wa Twita, imetangaza kifo cha mama mzazi wa kocha wao, Pep Guardiola, Dolors Sala Carrio, ambaye amefariki leo kwa ugonjwa wa virusi vya Corona akiwa na umri wa miaka 82.
Katika taarifa yake, Man City, imesema, imepokea kwa huzuni kubwa habari ya kifo hicho, huku akituma salamu za pole kwa Guardiola, familia yake, ndugu, jamaa na marafiki.