Home Mchanganyiko WANANCHI WAITIKIA WITO WA SERIKALI

WANANCHI WAITIKIA WITO WA SERIKALI

0

*******************************

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Leo Jumatatu Aprili 6, 2020 Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amewashukuru Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe kwa kuitikia vyema wito wa Serikali wa kupambana na ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na kirusi Corona.

Gavana Shilatu ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kukagua maeneo mbalimbali kuona namna gani Wananchi wanajikinga na ugonjwa wa virusi vya Corona ambapo alikuta Watu wengi wamezingatia somo la kunawa kwa kuweka ndoo yenye maji pamoja na sabuni ambapo Wananchi wananawa mara kwa mara maji yanayotiririka.

“Kiukweli inatia faraja sana kuona Wananchi wanaungana na Serikali yao kupambana na Corona kwa nguvu moja. Kwenye mapungufu madogo madogo tuliyoyaona tumewaelimisha zaidi. Nimewasisitiza waendelee kusikiliza na kufuata maelekezo ya Wataalamu wa Afya juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huu.” Alisema Gavana Shilatu.

Kwenye ziara hiyo Gavana Shilatu aliambatana na Watendaji kata na vijiji, Maafisa afya pamoja na Viongozi wa Serikali ya Halmashauri ya Kijiji kutembelea maeneo yanayotoa huduma kwa jamii kama vile kwenye maduka na masoko.