**********************************
Usomaji kwa mfumo wa kidijitali haimaanishi kupitia simu yako ya mkononi, kishikwambi au kompyuta. Ina maana ya kujenga uwezo wa kujifunza kwa kuwaunganisha walimu au wanafunzi popote walipo. Ni njia sahihi ya kujifunza inayoleta maana halisi.
Wazo la usomaji kwa njia ya kidijitali linalenga kuongeza ufanisi na kuboresha mazingira ya usomaji kwa wahusika kutumia nyenzo za kisasa. Lengo siyo kuachana na mfumo wa mafunzo ya darasani bali kuuboresha kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia.
Kwa kutumia njia ya usomaji wa Kidijitali, lengo ni kumsaidia mwanafunzi kupata stadi au maarifa yanayohitajika ili kuondoa wasiwasi kuhusu eneo na wakati wa kujifunza, halikadhalika kasi ya kujifunza na njia inayotumiwa na mwanafunzi.
Vodacom Instant schools, ni mfano halisi wa jukwaa la elimu linalowaunganisha wanafunzi na walimu popote walipo kwa kupata elimu kupitia mfumo wa njia ya masafa.
Mpango huu ni sehemu ya ajenda pana ya Vodacom yenye lengo la kuongeza ubora wa kujifunza kwa njia ya kidijitali nchini Tanzania.
Portal yetu ya elimu inajumuisha zana za elimu katika mfumo wa kidijitali ikiwa ni pamoja na mtaala wa shule za msingi na sekondari kupitia mfumo uliopitishwa kimataifa wa Khan Academy ambao unapatikana kupitia simu ya mkononi na kompyuta kwa wakati wote.
Faida za jukwaa hili ni muhimu haswa katika kipindi hiki ambapo ulimwengu unapambana na kuenea kwa ugonjwa wa COVID- 19 almaarufu kama CORONA. Wakati huu ambao jamii mbalimbali duniani zinashauriwa kujitenga kwa kuepuka kukaa kwenye misongamano na wakati
huo shule zikiwa zimefungwa kusoma hakutakiwi kusitishwa.
Vodacom kupitia uwekezaji wake mkubwa katika mtandao wa mawasiliano wenye miundombinu bora imechukua jukumu muhimu kuweka mazingira wezeshi kwa wateja wake wanaojiunga na portal ya Instant schools ili kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakiwa nje ya
darasa popote wanapokuwa na kwa kasi zaidi.
Hivi karibuni Vodacom kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), tumezindua awamu ya pili ya utoaji wa kompyuta zilizounganishwa na intaneti bure ikiwa ni katika jitihada zake za kukuza elimu ya dijitali shuleni nchini kote.
Chini ya ushirikiano huu jumla ya wanafunzi 81,500 katika shule 163 za msingi na Sekondari zitafikiwa hadi kufikia mwisho wa mradi ambapo ni mwezi Desemba mwaka huu.