Home Michezo RONALDO AACHA MIDOMO WAZI MASHABIKI WAKE BAADA YA KUPOST PICHA AKINYOLEWA NYWELE...

RONALDO AACHA MIDOMO WAZI MASHABIKI WAKE BAADA YA KUPOST PICHA AKINYOLEWA NYWELE NA MKEWE

0

***************************

Nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo, ame-post video katika ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi zaidi ya milioni 200, ikinyolewa nywele na mpenzi wake, Georgina Rodriguez, jambo ambalo limewaburudisha watu wengi.

Mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or, ameonekana mwenye furaha na kipenzi cha roho yake, wakati huu wa kujitenga na kukaa nyumbani kuepuka maambukizi ya virusi vya #Corona.

CR7 ameshindwa kwenda katika Saluni anayonyoa nywele ili kutekeleza agizo la serikali la kuwataka watu kukaa ndani.