Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Wilbert Ibuge na Balozi Nguyen Doanh wa Vietnam wakiangalia nyaraka mbalimbali walipokutana Ofisini jijini Dodoma kuzungumzia namna ya kuimarisha na kuboresha mahusiano ya kihistoria yaliyopo baina ya Tazania na Vietnam.
Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh (katikati) akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Col. Wilbert A. Ibuge (kulia) alipofika katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma kuitikia wito wa Katibu Mkuu kushoto ni afisa ubalozi wa Vietnam aliyefuatana na Mhe. Balozi Nguyen.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Col. Wilbert A. Ibuge katikati akimkaribisha Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu kulia ni Kaimu Mkurugenzi
anayeshughulikianchi za Asia na AustralasiaBw. Ceasar Waitara.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Col. Wilbert A. Ibuge (kulia) akizungumza na Balozi wa Vietnam chini Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara Jijini Dodoma alipofika kuitikia wito wa Katibu Mkuu
******************************
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Col. Wilbert A. Ibuge leo tarehe 26 Machi, 2020 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi
wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh katika ofisi za Wizara, Makao Makuu, Jijini Dodoma.
Balozi Doanh alikuja jijini Dodoma kufuatia wito wa Balozi Ibuge na kufanya mazungumzo yaliyohusu mambo mbalimbali kuhusu mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam, likiwemo suala la uwekezaji wa Vietnam nchini kupitia Kampuni ya simu ya Halotel.
Katika mazungumzo yao, viongozi hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano baina ya Nchi mbili hizo, ikiwemo uendelevu wa mawasiliano ya Kidiplomasia ambapo mahusiano ya Tanzania na Vietnam yamefikisha miaka 55 mwaka huu huku fursa za uwekezaji nchini zikiendelea kuimarishwa na hivyo kuiwezesha Serikali ya Vietnam ambayo ni mmiliki wa Kampuni ya Simu ya Halotel kuwekeza nchini na kuendesha shughuli zake.
Balozi Ibuge pia alimjulisha Mhe. Balozi Doanh kuwa Serikali ya Tanzania kupitia Wizara itaendelea kuhimiza uwekezaji kutoka Vietnam na kusisitiza uwekezaji huo kuzingatia sheria za nchi, kwa lengo la kuwepo tija kwa pande zote zinazohusika.
Kufuatia kikao hicho, Mhe. Balozi Doanh aliahidi kuendelea kuyasisitiza makampuni ya Vietnam Nchini ikiwemo kampuni ya Halotel kuzingatia Sheria, Taratibu na Kanuni
zilizowekwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha pande zote mbili zinanufaika.