RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar wakati alipotembelea jengo linalotarajiwa kuwa la Uchunguzi wa Virusi Zanzibar, Binguni Wilaya ya Kati Unguja leo.25/3/2020 (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Dkt. Mayasa Salum Ali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake kutembelea jengo linalotarajiwa kuwa la Uchunguzi wa Virusi Zanzibar, lililoko katika eneo la Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Binguni Wilaya ya Kati Unguja akielekea katika jengo hilo(kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Afya Zanzibar. Mhe. Hamad Rashid Mohamme.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar.Dkt. Mayasa Salum Ali, alipowasili katika viwanja vya Taasisi hiyo Binguni Wilaya ya Kati Unguja kutembelea jengo linalotarajiwa kuwa la Uchunguzi wa Virusi Zanzibar, (kushoto kwa Rais )Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Ayoub Mohammed Mahmoud na Waziri wa Afya Zanzibar. Mhe. Hamad Rashid Mohamed.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akiwa na Waziri wa Afya Zanzibar.Mhe. Hamad Rashid Mohammed, akiwa katika viwanja vya Taasisi ya Utafiti wa Afya Zanzibar Binguni Wilaya kati alipotembelea jengo linalotarajiwa kuwa la wa Virusi Zanzibar Binguni Wilaya ya Kati linaloonekana katika picha kwa nyuma.(Picha na Ikulu).
******************************
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kuacha ukaidi na kufuata kikamilifu maelekezo ya Serikali, ikiwa ni hatua za kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na Virusi vya Ugonjwa wa Corona.
Dk. Shein amesema hayo leo wakati alipotembelea eneo linalotarajiwa kujengwa jengo la Uchunguzi wa maradhi makuu, liliomo ndani ya taasisi ya Utafiti wa Afya, huko Binguni, Wilaya Kati Unguja.
Amesema katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa huo, Serikali tayari imetowa malekezo kadhaa, ikiwa njia ya kujikinga na virusi vya ugonjwa huo, hivyo akawataka wananchi kuacha ukaidi na kutekeleza maelekezo ya
kudumisha usafi kama inavyoelekezwa.
Alisema Virusi vya Ugonjwa wa Corona ni janga na Kimataifa na ni maradhi yasiotaka mzaha wala hayachaguwi aina ya mtu wa kuamuathiri, hivyo ni vyema wananchi wakaondokana na ushindani na kuzingatia maelekezo ya Serikali.
Alieleza kuwa Serikali imeingia katika vita dhidi ya adui asieonekana na hivyo ikalazimika kuchukuwa hatua mbali mbali za dharura ikiwemo kuzuia Kongamano la dini pamoja na kuzifunga skuli zote na wanafunzi kukosa
taaluma.
Shein alisema Serikali haiwezi kuainisha ukubwa wa gharama inazopoteza kutokana na hatua ilizochukuwa katika kukabiliana na virusi vya ugonjwa wa Corona, sambamba na athari za kiuchumi zitokanazo na kuvurugika kwa sekta ya utalii, ambayo huchangia asilimia themanini ya fedha za kigeni.
Rais Dk. Shein aliwataka wananchi kuondokana na upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa wananchi kuondokana na mikusanyiko, hususan katika eneo la Hospitali kuu ya Mnazi mmoja pamoja na maeneo ya masoko, kwa kigezo kuwa hatua hiyo inaweza kuwa chanzo cha kusambaa kwa viusi hivyo, pale itakapotokezea mtu mmoja kuwa navyo.
Katika hatua nyengine, Dk. Shein alilisistiza azma ya Serikali ya kujikita katika kufanya uchunguzi wa maradhi mbali mbali kwa kigezo kuwa hakuna tiba muafaka bila ya kuwepo uchunguzi, hivyo akabainisha dhamira ya
Serikali katika kukamilisha ujenzi wa jengo la kisasa la Maabara katika eneo hilo la Binguni.
Alisema Serikali imefikia uamuzi wa kukamilisha jengo hilo mahala hapo kwa kuzingatia mazingira bora yaliopo, ambayo yamejitenga na pia ni mazuri kwa shughuli hizo.
Aliwahakikishia wananchi kuwa jengo hilo litakamilika ndani ya kipindi cha miezi mitatu ijayo pamoja na kuwekewa vifaa vyote muhimu ili kukidhi mahitaji na malengo yaliokusudiwa.
Aidha, alisema Serikali itakamilisha miradi yote ya Maendeleo iliyokwisha anzishwa, ikiwemo ya ujenzi wa Nyumba Kwahani, Michenzani Mall, Barabara, Mahakama Kuu na mingineyo pamoja na kuanzisha miradi mipya, huku akibainisha kuwa endapo kutatokezea upungufu wa fedha itaangalia namna ya kukamilisha miradi hiyo.
Mapema, Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed, amesema Wizara hiyo imejiandaa kikamilifu kushirikiana na Serikali ya Watu wa China katika dhana ya kukuza utalaamu ili kuleta ufanisi wa maabara itakayojengwa.