Home Mchanganyiko KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAPITIA MAPENDEKEZO...

KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAPITIA MAPENDEKEZO YA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 KILICHOFANYIKA JIJINI DODOMA LEO

0

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (Katikati), Katibu Mkuu, Christopher Kadio (Kulia) na Naibu klatibu Mkuu, Ramadhani Kailima (Kushoto) wakizungumza kabla ya kuanza Kikao Cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Wizara hii imewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21 katika Kikao kilichofanyika
Jijini Dodoma leo.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (Kushoto), Katibu Mkuu, Christopher Kadio (Katikati) na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee (Kulia) wakizungumza kabla ya kuanza kwa Kikao Cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni Jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Christopher Kadio (Wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa Viongozi Wakuu wa Wizara hii kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
Wizara hii imewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21 katika Kikao kilichofanyika Jijini Dodoma leo.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, ,(wa kwanza kushoto ), akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama cha kupitia mapendekezo ya Bajeti ya
Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Christopher Kadio, (aliyesimama) akifafanua jambo wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kupitia mapendekezo ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ramadhani Kailima, (aliyesimama) akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakati wa Kikao cha kupitia mapendekezo ya Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kilichoketi kupitia mapendekezo ya Bajeti ya
Wizara hii kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika leo jijini Dodoma.

Baadhi ya Watendaji kutoka Jeshi la Magereza, Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Uhamiaji Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakiwa katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichoketi kupitia
mapendekezo ya Bajeti ya Wizara hii kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kilichofanyika leo jijini Dodoma.