Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd imekabidhi zawadi ya Katoni ya Juisi ya Matunda maarufu JAVIDA kwa Mfanyakazi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga mkazi wa Shinyanga Mjini aliyefanikiwa kujibu kwa ufasaha swali kuhusu maana ya JAVIDA.
Akizungumza leo Jumatano Machi 25,2020 wakati wa kukabidhi zawadi hiyo, Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa amesema Makalanga ni mshindi wa swali lililoulizwa na jambogroup katika mtandao wa Instagram.
“Kampuni ya Jambo Food Products kupitia mtandao wa Instagram katika akaunti ya jambogroup tumekuwa tukiuliza maswali mbalimbali na mfuasi ‘follower’ anayejibu kwa ufasaha huwa tunampatia zawadi na leo tunakabidhi zawadi kwa bwana Paul Makalanga aliyejibu vizuri maana ya JAVIDA ambapo JA-VIDA ni ufupisho wa (JAmukaya-VIDA); Jamukaya ikiwa na maana Ya Nyumbani (Sukuma), na Vida ikiwa na maana ya Maisha (Occitan). Ndiyo Maana JA-VIDA ni Utamu mpaka tone la Mwisho”,alisema Issa.
Aidha amewaomba wadau mbalimbali kuendelea kutembelea kurasa za JamboGroup katika mitandao ya kijamii ili kufahamu bidhaa zilizopo sokoni hali kadhalika kujibu maswali yanayoulizwa na kujipatia zawadi za Jamukaya ikiwemo Vinywaji baridi na tisheti.
Kwa upande wake, Paul Makalanga ameishukuru Kampuni ya Jambo Food Products kwa kumpatia zawadi ya Katoni ya Juisi ya JAVIDA ambayo ni bidhaa mpya iliyoingizwa sokoni hivi karibuni na Kampuni hiyo ya Vinywaji.
“Mimi ni Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises iliyoshiriki katika shindano katika Ukurasa wa Instagram lililokuwa linahoji maana ya JAVIDA. Nilijibu swali na kufanikiwa kulipata. Shukrani za dhati ziende katika Kampuni ya Jambo Food Products kwa kuniletea zawadi hii ya kinywaji kizuri na kitamu sana ambacho nina imani kuwa Watanzania wote watakipenda”,alisema Makalanga.
Kampuni ya Kampuni ya Vinywaji Baridi ya Jambo Food Products Ltd ya Mkoani Shinyanga hivi karibuni imetambulisha bidhaa mpya ya JAVIDA,Jawiza Apple Crush Soda,Juisi ya Ukwaju na Ubuyu zenye ujazo wa mili lita 300 ambazo zinapatikana kwa bei ya reja reja shilingi 500/= bei ambayo ni ya kizalendo kwa kila Mtanzania kwenye kipato cha kawaida.
Endelea kutembelea Ukurasa wa JamboGroup Instagram upate zawadi za Jamukaya JamboGroup
Kulia ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa akikabidhi zawadi ya Katoni ya Juisi ya JAVIDA”Utamu Hadi Tone la Mwisho” kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga mkazi wa Shinyanga Mjini aliyejibu kwa ufasaha swali kuhusu maana ya JAVIDA katika Ukurasa wa Instagram wa JamboGroup leo Jumatano Machi 25,2020. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kulia ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa akikabidhi zawadi ya Katoni ya Juisi ya JAVIDA”Utamu Hadi Tone la Mwisho” kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga mkazi wa Shinyanga Mjini aliyejibu kwa ufasaha swali kuhusu maana ya JAVIDA katika Ukurasa wa Instagram wa JamboGroup
Kulia ni Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa akikabidhi zawadi ya Katoni ya Juisi ya JAVIDA”Utamu Hadi Tone la Mwisho” kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga mkazi wa Shinyanga Mjini aliyejibu kwa ufasaha swali kuhusu maana ya JAVIDA katika Ukurasa wa Instagram wa JamboGroup
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa (katikati) na Mhasibu wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Erick Maro (kulia) wakikabidhi zawadi ya Katoni ya Juisi ya JAVIDA kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga mkazi wa Shinyanga Mjini aliyejibu kwa ufasaha swali kuhusu maana ya JAVIDA katika Ukurasa wa Instagram wa jambogroup leo Jumatano Machi 25,2020.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa (katikati) na Mhasibu wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Erick Maro (kushoto) na Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga (kulia) wakiwa wameshikilia juisi ya JAVIDA.
Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Products Ltd kwa kumpelekea zawadi ya Katoni ya JAVIDA.
Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga akionja Utamu wa JAVIDA….‘Utamu Hadi Tone la Mwisho”.
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Bi. Farida Issa (kushoto) na Mhasibu wa Kampuni ya Jambo Food Products Ltd, Erick Maro (kulia) na Mwakilishi wa Kampuni ya Gilitu Enterprises Ltd, Paul Kalanga (kushoto) wakiwa wameshikilia juisi ya JAVIDA.
JAMUKAYA JAVIDA ….’Utamu Hadi Tone la Mwisho”
Ujumbe wa jambogroup katika ukurasa wa Instagram ikimtangaza gilitu_enterprises_ltd kuwa mshindi wa swali kuhusu maana ya JAVIDA.