Home Mchanganyiko HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU YASHIRIKIANA NA WANAKIJIJI WAKE KUPANDA MITI 2900

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU YASHIRIKIANA NA WANAKIJIJI WAKE KUPANDA MITI 2900

0

Tunachapa kazi na kuzingatia tahadhali zote juu ya CoronaVirus. Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga(mwenye kofia) na Mratibu wa Mradi wa MVIWATA Donald Laizer.

*******************************

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga akishirikianana Wanakijiji cha Dongobesh kupanda miti 2900 ili kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakishirikiana na Wadau mbalimbali wamepanda miti mbalimbali na hasa miti asilia inayokwenda sambamba na hali ya hewa yaWilaya hiyo.

“Tumeshajiwekea Mkakati na Kampeni ya Kupanda katika maeneo yote halmashauri ya Mbulu yenye vilima namiinuko iliyo wazi ili kuweka urithi bora kwa kizazi cha sasa na baadae” alisema Hudson Kamoga.

Pamoja na Upandaji wa Miti ya Mbao,pia alisisistiza wananchi kuandaa na Kupanda miti ya Matunda.

Naye Mratibu wa MVIWATA Manyara, Ndugu Donald Laizer na amashukuru Mkurugenzi kwa ushirikiano anaoupata nakuahaidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika uboreshaji wa Mazingira.