Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
NA FREDY MGUNDA,MUFINDI.
Wakala wa Misitu Tanzania TFS kupitisha Shamba la Miti Sao Hill Wilayani Mufindi mkoani Iringa Limewahimiza wananchi kuendelea kuitunza misitu iliyopo katika maeneo yao na kuitumia kuwa fursa ya kiuchumi kwa kizazi cha sasa na baadae.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea Siku ya Misitu Duniani ambayo huadhimishwa Tarehe 21 ya mwezi wa Tatu ya kila mwaka, Meneja wa Shamba la Miti Sao hill Juma Mseti amesema utunzaji wa misitu hiyo utaendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi kwa Taifa, pamoja na kutoa ajira mbalimbali kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya misitu hiyo.
Alisema kuelekea maadhimisho hayo wameendelea kusisitiza juu ya utanzanji wa mazingira na uhifadhi wa misitu ikiwemo ya Sao hill kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa manufaa ya jamii nzima.
Mseti alizungumzia juu ya faida za uhifadhi wa misitu meneja Juma Mseti amesema licha ya kuwa chanzo cha ajira kwa jamii, pia misitu ni sehemu ya makazi ya wanyama, husaidia katika ulinzi wa vyanzo vya maji pamoja na kuzuia mmomonyoko wa Udongo.
“Maadhimisho ya siku ya misitu ufanyika Machi 21 kila mwaka huku nchi mbalimbali Duniani zikihimizwa kuendeleza juhudi za kitaifa na kimataifa ili kuandaa na kushiriki katika shughuli zinazohusika na misitu pamoja na miti, kama vile kampeni ya kupanda miti pamoja na midahalo kuhusu misitu. Siku hii huadhimishwa kwa ajili ya kuwafanya watu waelewe umuhimu wa aina zote za misitu duniani, ikiwemo jukumu lake katika mabadiliko ya tabia nchi” alisema Mseti
Tamko la Umoja wa Mataifa linaiomba Sekretarieti ya Jumuiko la Umoja wa Mataifa juu ya Misitu (UNFF), kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), kufanikisha utekelezaji wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Misitu, kwa kushirikiana na Serikali, pamoja na wadau wa Masuala ya Misitu wakiwamo Sao hill na taasisi mbalimbali
Kauli mbiu iliyochaguliwa kwa mwaka 2020 juu ya maadhimisho ya siku ya misitu Dunia “MISITU BIOANUWAI NI TUNU NA TUILINDE”