Home Mchanganyiko MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGONJWA YA RHRUMATISM KWA WATOTO DUNIANI

MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGONJWA YA RHRUMATISM KWA WATOTO DUNIANI

0

Daktari bingwa wa magonjwa ya Rheumatism katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk Francis Furia akizungumza katika maadhimisho hayo

********************************

Na Magreth Mbinga

Tarehe 18 march kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya magonjwa ya Rheumatism lengo likiwa kuongeza ufahamu wa jamii kuhusiana na magonjwa ya Rheumatism kwa watoto.

Hayo yamezungumzwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya Rheumatism wa hospitali ya taifa ya Muhimbili Dk Francis Furia katika maadhimisho ya siku ya magonjwa ya watoto ya Rheumatism duniani .

Pia amesema magonjwa haya yana changamoto kubwa ya kugundulika haraka kwakuwa mengi hayana vipimo maalumu vinavyoweza kupima na kusema moja kwa moja.

“Magonjwa haya ya Rheumatism husababishwa na hitilafu katika mfumo wa kinga ya mwili ambayo hushambulia sehemu mbalimbali za mwili badala kuulinda,magonjwa haya yanaweza kusababisha ulemavu na udhaifu wa mwili” amesema Dk Furia.

Vilevile amesema baadhi ya magonjwa ya Rheumatism ni Ugonjwa wa viungo,Ugonjwa wa Lupus,Ugonjwa wa Moyo,Ugonjwa wa misuli na Ugonjwa wa ngozi na magonjwa haya ya Rheumatism husababisha ulemavu kwa kiasi kikubwa.

“Walengwa wakubwa katika siku hii ni watoto,wazazi,na wahudumu wa afya wazazi wanapewa elimu ili kuwahi kuwapeleka watoto hospitali ambapo wataanza matibabu mapema na kupunguza uwezekano wa kupata madhara ya magonjwa haya ikiwemo ulemavu wa Viugo” amesema Dk Furia.

Amemalizia kwa kusema elimu hii ya afya ni muhimu kwa wahudumu wa afya kwakuwa magonjwa haya hufananishwa na magonjwa ya kuambukizwa ikiwemo virusi vya ukimwi(VVU) na kifua kikuu na magonjwa hupatiwa matibabu ambayo siyo stahiki pia ucheleweshwa kupata rufaa.

“Kliniki ya magonjwa haya inapatikana katika hospitali ya Taifa Muhimbili na pia huduma zinatolewa katika hospitali nyingine kwa uahirikiano na madaktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili wazazi wapeleke watoto wao kupata huduma na wasipopata nafuu waombe rufaa kuja katika hospitali za ngazi za juu zaidi” amesema Dk Furia.