WAZEE WA KIMILA MKOA WA SINGIDA WAOMBWA KULIOMBEA TAIFA LISIKUMBWE NA UGONJWA WA CORONA
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Mbua Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa .
Wazee wa kimila wakiwa kwenye mkutano wa Meya.
Wazee wa kimila wakimkabidhi Meya zana za kimila.
Na Mwadishi wetu, Singida
WANANCHI wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona ambao unaonekana kuwa tishio na janga la kidunia.
Meya wa Manispaa ya Singida, Alhaji Mbua Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya ilani ya uchanguzi kwenye kata hiyo ya miaka mitano ya utekelezaji wakati alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara.
“Nawashukuru sana wananchi kwa kuniunga mkono katika kipindi cha miaka mitano ya utekelezi wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa pamoja tumeweza kufanya mambo mbalimbali ya maendeleo hasa katika kata yetu hii-tumeweza kutatua changaomoto mbalilmbali kama maji, elimu, barabara, afya na kuwapatia mikopo vikundi vya kinamama na vijana zaidi ya milioni kumi na saba zimetolewa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.” alisema
Aidha Meya ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuipatia kituo cha afya kata hiyo ambacho kinatoa huduma bora kwa wananchi na kuondoa malalamiko yaliyokuwepo awali.
“Nimejaribu kuunga mkono shughuli mbalimbali za kijamii kama diwani wenu, nimetoa mipira kwenye shule zetu zote, nimechangia zaidi ya milioni moja kwenye maendeleo ya kata yetu katika nyaja mbalimbali.”alisema Meya
Hata hivyo Meya huyo amewakumbusha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari pamoja na wale wenye imani kuendelea kumuomba mwenyezi Mungu na wazee wa kimila kuingilia kati ili kuzuia janga la ugonjwa wa corona.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Boniphace Ipini amesema kwa kushirikiana na watendaji wa vjiji wanaendelea kuchukua tahadhari hasa kwenye minada ambapo kunakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Tunatengenza mabango ya kutoa ujumbe wa tahadhari ya ugonjwa huu na tutatenga sehemu za kunawia mkono katika maeno yote ya mikusanyiko ya watu na maofisini.
Kwa upande wao wananchi wamemshukuru sana diwani huyo ambapo wamesema amejitahidi kutimiza ahadi zake japo hajazimaliza zote.
“Tunamshukuru Rais wetu Dkt. John Magufuli kwa kutuletea kituo cha afya na wataalamu kwasasa tunapa huduma bora na kwa wakati tofauti na mwanzoni.” walisema wananchi.