Home Michezo WATOTO ZAIDI YA 35 WAMESHIRIKI MASHINDANO YA TANAPA LUGALO OPEN

WATOTO ZAIDI YA 35 WAMESHIRIKI MASHINDANO YA TANAPA LUGALO OPEN

0

**********************

WATOTO ZAIDI YA 35 WAMESHIRIKI MASHINDANO YA TANAPA LUGALO OPEN AMBAPO MTOTO KARIM ISMAIL  AMEONGOZA KWA KUPATA MIKWAJU 69 HUKU MTOTO MWENZIE HAMADI MAULIDI AKISHIKA NAFASI YA PILI KWA KUPATA MIKWAJU 70 NA UPANDE WA WANAWAKE SHUFAA TWALIBU AKIONGOZA KWA KUPATA MIKWAJU 90.

WAKIZUNGUMZA BAADA YA KUMALIZA MCHEZO HUO ULIOHUSISHA WATOTO 20 AMBAO WALICHEZA VIWANJA VYOTE 18 WATOTO HAO WALIOONGOZA WAMESEMA MCHEZO HUO ULIENDA VIZURI INGAWA KULIKUA NA CHANGAMOTO CHACHE UWANJANI ILA WANATARAJIA KUFANYA VIZURI ZAIDI KWENYE MASHINDANO MENGINE YAJAYO.

KWA UPANDE WA WACHEZAJI WA KULIPWA MCHEZAJI WA KLABU YA GOFU ARUSHA JOHN LEONS AMEIBUKA MSHINDI KWENYE MASHINDANO HAYO AMBAPO AMESEMA SIRI YA USHINDI WAKE NI MAZOEZI YA MARA KWA MARA NA KUSHIRIKI KWENYE MASHINDANO MBALIMBALI.

MASHINDANO YA TANAPA LUGALO OPEN YALIANZA RASMI MARCH 13 MWAKA HUU KWA WACHEZAJI WA KULIPWA,MARCH 14 HADI MARCH 15 KWA WACHEZAJI WA RIDHAA NA WATOTO AMBAPO WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO DR HARRISON MWAKYEMBE ATAKUA MGENI RASMI KATIKA UTOAJI WA ZAWADI KWA WASHINDI.