Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Bw.Alban Kihula akiwaelekeza wabunge namna ya upimaji matenki ya mafuta kwa kutumia Stiki, Baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Bw.Alban Kihula akiwaelekeza wabunge namna ya upimaji wa mita za dira ya maji kabla ya matumizi kwenye mabomba ya maji, Baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Viwanda,Biashara na Mazingira kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
Meneja Wakala wa Vipimo Mkoa wa Pwani, Bw.Alban Kihula akiwaelekeza shughuli ambayo wanaifanya katika kituo hicho Baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira kutembelea kituo cha Wakala wa Vipimo Misugusugu Mkoa wa Pwani.
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kamati ya kudumu ya Bunge ya viwanda,Biashara na Mazingira limefurahishwa na utendaji kazi wa Kituo cha Wakala wa Vipimo WMA-Misugusugu Mkoa wa Pwani baada y kutembelea kituo hicho na kujiona utendaji kazi.
Akizungumza katika Kituo hicho Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Suleiman Sadick Murad amesema kuwa kituo hicho mpaka sasa kimefanya kazi kubwa kwani mpaka wamejiweka kisasa zaidi hususani kuelekea Tanzania ya Viwanda.
“Tumetembelea eneo hili la Kituo tumejionea zile changamoto ambazo tulikuwa tunaziona kule mjini Dodoma sasa leo tumepata majibu kwani tumeuliza maswali ya kutosha na kujibiwa vizuri”. Amesema Mhe.Murad.
Aidha Mhe.Murad amesema kuwa wameona mita za dira ya maji na kuelimishwa juu ya upimaji wa mita hizo kwani mita kabla ya kwenye mamlaka kama DAWASCO,MOROWASA na nyinginezo lazima kwanza ipitie kwenye kituo kwaajili ya vipimo.
“Katika uletaji wa mita hizo kinachosemekana watu wanaleta sampo nzuri baadae wanaleta mita ambazo hazina viwango na hili limetokea leo hapa kuna mita nyingi hazifai”. Ameeleza Mhe.Murad.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu (WMA), Dkt.Ludovick Manege kwenye suala la upimaji mita za maji amesema kuwa mpaka sasa kituo hicho kina mwaka mmoja tangu kianze shughuli hiyo na hadi sasa wameshapima takribani mita za dira ya maji laki 4 na kuweza kukuta mita ambazo hazifai kwa matumizi 530.
Pamoja na hayo Dkt.Manege amesema kuwa wamekuwa wakipima magari ya mafuta pia kwani mpaka sasa wameweza kupima magari ya mafuta takribani 4554.
“Mpaka sasa tumeshapima magari takribani 4554 na katika magari hayo tumeweza kukuta magari takribani 200 ambayo yanakasoro na kuwataka waende wakayarekebishe warudi tena kuyapima pia kwa kutwa tunapima magari 70”. Amesema Dkt.Manege.