Home Mchanganyiko Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi wa Ubelgiji, Sweeden

Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi wa Ubelgiji, Sweeden

0

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimueleza jambo Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao jijini Dar es Salaam

Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter
Van Acker wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

************************

Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker pamoja na Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg.

 

Mazungumzo ya Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.

 

Balozi wa Ubelgiji, Mhe. Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako kinachopatikana
katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

 

"kupitia uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za
ajira kwa mataifa haya mawaili," Amesema Balozi Acker.

 

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Tanzania itahakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara. Katika tukio jingine, Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Mhe. Anders Sjoberg,

 

ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia. Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa Sweeden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinapiga hagtua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

 

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendeleza kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na Sweeden katika Sekta mbalimbali hasa katika wakati huu ambao Tanzania inapiga hatua kuelekea uchumi wa viwanda.