SERIKALI ya wilaya ya Iringa imepiga marufuku sherehe zote harusi ambazo hazina kibali maalumu kutoka kwa Mganga mkuu wa wilaya (DMO) kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya virusi vya Corona nchini.
Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya afya,mkuu wa wilaya ya iringa Richard kasesela alisema kuwa sherehe zote za harusi haziruhusiwi kufanyika bila kupata kibari maalumu kwa lengo la kulinda afya za wananchi wanaokuwa wanasherekea harusi kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya virusi vya corona.
Ni lazima kila sherehe katika wilaya ya Iringa kuwepo mfumo wa kusafishia mikono kwa lengo la kukwepa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa tishio hapa nchini na duniani kwa ujumla.
Kasesela alisema kuwa kwenye harusi huwa kuna kuwa na mkusanyiko wa watu wengi hivyo ni lazima kuweka king a mapema ili yasitokee maambukizi makubwa kama ambayo yametokea nchi nyingine.
Aisha kasesela aliwataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuwa makini na mikusanyiko ya watu ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa vinatishia uhai wa wananchi.
“Misiba,kusalimia,vituo vya usafiri,makanisani na misikitini ni lazima kuondokana na Mira na tamaduni zetu ambazo tumekuwa tumezizoea ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya corona” alisema kasesela
Kasesela alitaka halmashauri zote za wilaya ya Iringa kuhakikisha kwenye vituo vya afya,vituo vya mabasi,maduka makubwa,kampuni mbalimbali zote lazima kuwe na sehemu za kunawia mikono ili kuepuka na maambukizi ya virusi vya corona.
“Iringa hakuna hata mgonjwa mmoja wa maambukizi ya virusi vya corona na taarifa zinazoenea sio za kweli wananchi wa iringa wanatakiwa kuzipuuza na mwenye jukumu la kutangaza uwepo virusi hivyo ni waziri husika au viongozi wa ngazi za juu”alisema kasesela
Kwa upande wake mdau wa sekta ya afya mkoani Iringa Ahmed Asas alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa waandishi wa habari,wafanyakazi wa kampuni ya Asas na taasisi binafsi kwa lengo la kuepuka kuambukizwa virusi vya corona.
Ahmed alisema kuwa kwenye kampuni ya Asas wamefanikiwa na kuwa na chumba maalumu kwa ajiri ya wafanyakazi watao kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya corona na wameganikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi kwa lengo la kuwa msaada kwa wafanyakazi wengine.
“Sisi tupo tayari kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona sehemu yeyeyo ile kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kama ambavyo yumeanza na mkuu wa mkoa wa Iringa Richard kasesela” alisema Ahmed
Naye mganga mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Samwel Marwa alisema kuwa wamejipanga kila idara kuhakisha wanatoa elimu na kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.