Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkuu wa Kitivo cha
Sheria Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. John Ubena mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akitoa taarifa kwa Waziri kuhusu
maendeleo ya Chuo
Wataalamu wa kitivo cha Sheria wakimsikiliza Waziri
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi.Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na wanataaluma wa Kitivo
cha Sheria wa Chuo Kikuu Mzumbe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo ya awali ya lengo la
ziara
Waziri akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wahadhiri wa Sheria Chuo kikuu Mzumbe.
******************************
Chuo Kikuu Mzumbe kimepongezwa kwa umahiri wake katika ufundishaji masomo ya sheria, na kuwa
Chuo bora chenye wahitimu mahiri na wajuzi kwenye fani ya Sheria nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza, tangu ameteuliwa kushika nafasi hiyo; akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na baadhi ya watendaji kutoka taasisi na Idara za Sheria zilizopo chini ya Wizara hiyo.
Pamoja na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe, amewataka kuongeza ubunifu zaidi katika kutoa wanafunzi bora, kwa kuzingatia miiko ya kazi ili kuwaandaa vijana wenye nidhamu na weledi.
Chuo Kikuu Mzumbe ni Chuo cha Umma kinachotoa kozi mbalimbali za Sheria kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), Shahada ya Awali (Degree) na Shahada za Umahiri (Masters) katika Sheria.