******************************
Happy Lazaro,Arusha.
JESHI la Polisi mkoani Singida limeishukuru Kampuni ya Sunny Autoworks Ltd na Sunny Adventure Safaris kwa kuwasaidia kukarabati magari mawili ya jeshi hilo, kati ya matatu yaliyotolewa na jeshi kwa ajili ya matengenezo.
Akizungumza jijini Arusha, wakati akipokea magari hayo toka kwa Mkurugenzi wa kampuni hiyo,Ayub Ali Haji Suleman,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Sweetbert Njewike alisema kutengemaa kwa magari hayo kutaongeza utendaji kazi wa jeshi hilo katika kudhibiti uhalifu wakati was kufanya doria .
“Hakika tunaishukuru kampuni ya Sunny Autoworks LTD na kampuni ya utalii ya Sunny Adventure Safaris kwa kututengenezea magari yetu na kutukabidhi yakiwa mapya,”alisema.
Njewike alisema kazi kubwa ya polisi ni kufanya doria fupi na za masafa marefu ili kuhakikisha amani,usalama na utulivu unakuwepo kwa wananchi.
Aidha alisema ili kufanikisha kufanya doria hizo ni lazima wawe na vyombo vya usafiri kama pikipiki,magari na vingine.
Alisema kwa sasa Mkoa wa Singida upo shwari tofauti na miaka ya nyuma kulivyoshamiro matukio ya utekajj wa magari.
Mkurugenzi wa Sunny Works LTD na Sunny Adventure Safaris LTD, Ayub Alihaji Suleman alisema kampuni yake kwa zaidi ya miaka 30 wanajitolea kukarabati magari ya polisi na kikosi cha Zimamoto mkoani humo ili kuimarisha ulinzi.
“Sisi tunakarabati bure kama haya magari ingekuwa kutoa fedha yangegharimu zaidi ya Sh.milioni 20 lakini tunathamini mchango wa askari wetu na ndo maana tunayatengeneza bure,”alisema.
Alimshukuru pia Rais John Magufuli kwa kuzidi kudumisha amani na usalama nchini na kuwawezesha kufanya kazi zao bila shid