Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbweni aliofika kusikiliza na kutatua kero zao.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo akiwa ameambata na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi. Stella Msofe na viongozi wengine wakata na mitaa, wakitoka kukagua bandari kavu ambayo leo hii ameizindua rasmi.
Wananchi wa Kata ya Mbweni , wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo alipofika kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero zao.
******************************
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Daniel Chongolo amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Vizuri vya Corona ikiwa ni pamoja na kupokea wageni wasio wajuwa bila kuwa na uhakika wa afya zao.
Mhe. Chongolo ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa kwenye mkutano na wananchi uliokuwa na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali hivyo kuwataka kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake sambamba na kuepuka kukaribisha wageni kienyeji.
Ameongeza kuwa “ kuanzia leo nyinyi wenyewe muwe walinzi wa wenzenu, chukueni tahadhari, msije kupokea wageni wa aina yoyote ile kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kutumia njia mbalimbali za kuleta vizuri hivyo katika maeneo yetu” amesisitiza Mhe. Chongolo.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amezindua Bandari Bubu iliyopo Mbweni nakuzitaka Malaka za Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuepusha changamoto kwa wananchi, wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo.
Mhe.Chongolo amesema kila mamlaka husika zinapaswa kuwepo katika eneo pamoja na Taasisi nyingine ili kuwezesha wananchi na wafanyabiashara wanaotumia bandari hiyo kufanya shuguli zao kwa urahisi kulingana na mazingira rafiki yaliyopo.
Amefafanua kuwa Nchi ilikuwa inakosa mapato mengi kupitia upitishaji wa magendo katika maeneo ya fukwe za Mbeni, Ununio, Kunduchi pamoja na maeneo mengine ya pembezoni mwa fukwe za bahari na hivyo kueleza kuwa tayari bandari hiyo imeruhusiwa kutumika na watu kufanyabishara zao.
”hapo awali tulikuwa hatupati fedha kwenye hii Bandari, ila hivi sasa tumeanza kupata fedha , naomba tushirikiane vizuri na nikiondoka hapa kwenye mkutano , mamlaka zote ambazo zinapaswa kuwepo hapa ziwepo ikiwemo TRA, tunataka mapato wao wasiwe kikwazo cha kutukosesha mapato.
Katika hatua nyingine Mhe. Chongolo amemtaka OCD wa Kawe kuhakikisha kuwa usalama kwa wafanyabiashara unakuwepo sambamba na kuwachukulia hatua wote ambao watakiuka na kushindwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.