Home Mchanganyiko IGENI MFANO WA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA

IGENI MFANO WA UJENZI WA MAJENGO YA MAHAKAMA

0

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa pili kulia) akizungumza leo na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Loatha Sanare kuhusu ziara ya Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria kwa ajili ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.

 Jengo   la sasa la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, linalotumika  lililopo katika Wilaya ya Morogoro.

Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria  wakitoka kukagua leo  jengo la sasa la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro.

Muonekano wa jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu.

 Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria  wakiingia  kukagua leo  jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wa pili kushoto ni  Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria, Mhe. Emmanuel Mwakasaka  na (wa tatu kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Augustine Mahiga, wa (kwanza kushoto) ni  Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa   Majengo  ya Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja  leo na Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria mara baada ya wajumbe hao kutembelea jengo jipya la Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo Wilaya ya Morogoro. Wengine ni baadhi  ya viongozi wa Mahakama ya  Tanzania.

(Picha na Magreth  Kinabo – Mahakama)

***************************************

Na Magreth Kinabo – Mahakama

Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria imesema taasisi nyingine za umma zinapaswa kuiga mfano wa ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Tanzania,   kujenga majengo yao ili kuweza   kuyajenga vizuri  kwa kipindi kifupi.

Akizungumza leo mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo jipya la  Mahakama ya Mwanzo ya Ngerengere, lililopo katika Wilaya ya Morogoro, ambalo linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu,  Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya  Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria, Mhe. Emmanuel Mwakasaka alisema  majengo ya Mahakama yaliyojengwa  ni mazuri na yanajengwa kwa muda mfupi.

‘‘Tumetembea sehemu nyingi majengo ni mazuri yanapaswa kuigwa, Tunaomba mmfikishie salamu Rais kuhusu ujenzi huu wa majengo ya Mahakama, Tunampongeza,’’ alisema  Kaimu Mwenyekiti huyo.

Awali akizungumzia kuhusu ujenzi wa jengo hilo jipya, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa   Majengo  ya Mahakama ya Tanzania, Mhandisi Khamadu Kitunzi, alisema linachangamoto ya umeme ambapo na linatarajiwa kufungwa taa hivi karibuni.

Aliitaja changamoto nyingine  ni  maji ambapo wanatarajia kuchimba kisima. Hivyo jengo hilo  linatarajiwa kuanza kutumika rasmi Aprili 15, mwaka huu.

Kamati hiyo, ilianza ziara ya kikazi kwa ajili ya kukagua baadhi ya majengo ya Mahakama, Machi 12, mwaka huu, ambapo imekagua miradi ya ujenzi wa majengo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara na Mahakama ya Wilaya ya Kondoa. mradi wa ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Longido lililopo mkoani Arusha.

Pia imemaliza  ziara hiyo na  kuondoka leo mkoani Morogoro kuelekea Jijini Dodoma, ambapo inatarajia kufanya majumuhisho kesho kutwa.