Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege Enock Walter akizungumza namna walivyopokea elimu iliyotolewa na TCRA katika Shule hiyo.
Afisa Masoko wa TCRA Dorice Muhimbila akimkabidhi zawadi mwalimu kutokana na kujibu swali kwa usahihi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Mwandamizi Robson Shaban akitoa maelezo namna wanavyosimamia mawasiliano pamoja na utoaji elimu.
Afisa Masoko wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dorice Muhimbila akitoa mada kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani kuelekea kilele cha maadhinisho ya Siku walaji wa Huduma za Mawasiliano ambayo hufanyika kila Machi 15 ya Kila mwaka.
****************************
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa katika matumizi ya mitandao kuacha kuweka vitu binafsi katika mitandao.
Akizungumza wakati wa utoaji elimu ya kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Mwandege wilayani Mkuranga mkoani Pwani Afisa Masoko wa Mamlaka hiyo Dorice Muhimbila amesema kuwa Wanafunzi ni muhimu kuwa elimu hiyo ili wakianza kumiliki simu waweze kutumia mawasiliano hayo salama.
Muhimbila amesema kuwa elimu hiyo wanayoitoa ni kuelekea kilele cha maadhinisho ya Siku Walaji wa Huduma za Mawasiliano ambayo huadhimishwa kila Machi 15 ya Kila Mwaka
Amesema kuwa kuna sheria ya makosa mitandao hivyo wanafunzi wanatakiwa kupewa muongozo ili mwisho wa siku wasiweze kuangukukia katika mikono ya sheria wakati wa kutumia mawasiliano.
Muhimbila amesema kuwa TCRA imejipanga katika utoaji wa elimu katika makundi yote katika kuhakikisha wananchi wanatumia mawasiliano kwa usalama.
Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Mhandisi Mwandamizi Robson Shaban amesema kuwa wanafunzi wakipata elimu wanakuwa mabalozi kwa jamii nzima.
Amesema katika kipindi hiki teknolojia ya mawasiliano inakua hali ambayo lazima iendane na utoaji elimu.
Nae Mkuu wa Shule hiyo Enock Walter amesema kuwa elimu waliyoitoa katika Shule hiyo ni kubwa kwani hata walimu itawasadia katika utumiaji wa mawasiliano.
Aidha amesema TCRA waendelee kuwafikia mara kwa mara kuweza kupata elimu ya mawasiliano hasa kwa wanafunzi ambao ndio watarajiwa wa kutumia mawasiliano.