**********************************
Nteghenjwa Hosseah, Chato
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu OR-TAMISEMI Gerald Mweli amesema ameridhishwa na kutambua jitihada zinazofanywa na viongozi wa Wilaya ya Chato katika kuwekeza kwenye miundombinu ya Elimu.
Mweli ameyasema hayo wakati alipotembelea Wilaya hiyo na kukutana na Menejiment, Walimu pamoja na kukagua ujenzi wa shule mbalimbali zilizoboreshwa na zinazoendelea kuboreshwa Wilayani hapo.
Mweli amesema natambua jitihada kubwa mnazozifanya katika eneo hili la Elimu, naona mmejiongeza kwa kuanzisha kiwanda cha matofali ambayo yatatumika katika ujenzi wa madarasa hii ni jitihada nzuri sana katika kukuza sekta ya Elimu Wilayani Chato.
‘Naona mmeshafyatua matofali zaidi ya elfu tano na kazi inaendelea hii inanitia moyo; Kazi hii mnayoifanya itasaidia katika kupunguza gharama za ujenzi wa darasa hapa Chato kushuka kutoka Milioni 20 mpaka Milioni 10 kwa darasa moja kwahiyo kupitia mlango huu mtaweza kujenga madarasa ya kutosha’
Wilaya hii inawatoto wengi ambao wako shuleni na wengine wanakaribia kuanza shule hii inapelekea mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa ili watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaende na wapatiwe elimu bora aliongeza Mweli.
Katika kikao chake na Menejiment ya Halmashauri ya Wilaya Chato Mweli alisisitiza ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo kwa mwaka huu wa Fedha halmashauri hiyo inatakiwa kukusanya Bil 2.9 pia alipokea taarifa ya utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu.
Aidha wakati akizungumza na Walimu Mweli alitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na kutokea ufafanuzi katika kupanda madaraja kuwa kigezo si muda tu bali ninutendaji kazi, namna ulivyopimwana kwenye Opras pamoja mahitaji ya nafasi hiyo kwa wakati husika.
‘Alisisitiza kuwa kupanda madaraja sio kufikisha muda tu kuna sifa nyingi za ziada zinazoangaliwa kama hujazifikia zotr huwezi kupanda hata kama muda wako umefika hivyo tunatakiwa kujituma na kuleta matokeo katika maeneo yetu ya kazi wakati wote’ alisisitiza Mweli.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliud Mwaiteleke amesema halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha inakuanya mapato ipasavyo na fedha hizo zinaenda kutekeleza miradi ya maendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.
Pia aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi kama vile Mashine za kukusanyia mapato (POS) 43 ambazo kwa kiasi kikubwa zimedhibiti upotevu wa mapato.
‘Akitaja mikakati mingine waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato Mwaiteleke amesema ni kuanzisha kiwanda cha kufyatua matofali ambacho kimeshaanza kufanya kazi, ofisi ya kurudisha (Printing Unit) pamoja ufugaji.
Katika utoaji wa Mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Mwaiteleke amesema wamefungua akaunti maalumu ya Mikopo hiyo kwa mujibu wa maelekezo na kwa mwaka wa fedha uliopita mikopo iliyotolewa ni shilingi mil 117 sawa na asilimia 87 ya malengo waliyojiwekea.
‘Kwa mwaka huu wa fedha mikopo iliyotolewa katika robo ya kwanza ni shiling mil 51 zaidi ya lengo la kutoa Mil 50 iliyowekwa na kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walitoa shilingi Mil 78 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vingine ‘ aliongeza Mwaiteleke.
Mahitaji ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato ni 2257 kwa shule za Msingi na Sekondari na hii kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo katika Wilaya hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Mweli akiwa Chato alitembelea kiwanda cha halmashauri cha kufyatua matofali mfungamano (Interlock) shule ya Msingi Chato na Magufuli, shule ya sekondari Magufuli pamoja na Buselesele.