Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela kukagua miundombinu ya barabara kufuatia mvua zinazoendelea kunyessha ambapo amewaelekeza wakandarasi wawepo maeneo yote korofi ili kufanya marekebisho ya haraka.
Eneo la Kanga ambalo miundombinu ya barabara imeharibiwa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha maji kujaa barabarani, aidha mkandarasi Sanka Building and Civil Engineering ameelekezwa kufanya marekebisho kwa kujaza mawe ili eneo hilo lipitike kwa urahisi.
Eneo la Kanga ambalo miundombinu ya barabara imeharibiwa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha maji kujaa barabarani, aidha mkandarasi Sanka Building and Civil Engineering ameelekezwa kufanya marekebisho kwa kujaza mawe ili eneo hilo lipitike kwa urahisi.
Eneo la Kanga ambalo miundombinu ya barabara imeharibiwa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha, aidha mkandarasi Sanka Building and Civil Engineering ameelekezwa kufanya marekebisho kwa kujaza mawe ili eneo hilo lipitike kwa urahisi.
**************************
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amewaagiza wakandarasi kuwepo masaa 24 katika maeneo yote ya barabara yaliyoharibika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea ili kufanya marekebisho ya haraka pale inapobidi.
Akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Brig. Jen. Mwangela ametoa agizo hilo mara baada ya kukamilisha kwa ukaguzi wa barabara zote za Mkoa wa Songwe zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara Mijini (TANROADS) ili kufanya tathmini ya hali ya barabara Mkoani hapa.
“Barabara zote zina wakandarasi waliokuwa wanaendelea na matengenezo ila walisitisha kufuatia mvua kubwa hivyo nawaagiza wapepo masaa 24 katika maeneo yote korofi kuhakikisha tatizo linapotokea wanarekebisha haraka na barabara ziweze kuendelea kutumika.”, amesisitiza Brig. Jen. Mwangela.
Amesema mpaka sasa mvua bado ni tishio kwakuwa baadhi ya maeneo miundombinu ya barabara imeharibika vibaya huku TANROADS wakishindwa kufanya ukarabati kufuatia mvua hizo hivyo wakandarasi wajikite katika kuweka mawe ili ziweze kutumika na baada ya mvua matengenezo yaendelee.
Brig. Jen. Mwangela ametoa tahadhari kwa watumiaji wa barabara Mkoani Songwe kuwa endapo watakuta maji yamejaa barabarani wasivuke mpaka watakapo jiridhisha kina cha maji hayo huku akitaja baadhi ya maeneo korofi kuwa ni Nkanga Halmashauri ya Wilaya ya Songwe na Msangano halmashauri ya Wilaya ya Momba.
Ameongeza kuwa wazazi na walezi wasiwaruhusu watoto kucheza, kuvuka au kuogelea katika mito bila usimamizi wao kwakuwa mvua zinazoendelea kunyesha zimepelekea maji kuongezeka katika mito na baadhi ya maeneo ya makazi ya watu.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini (TANROADS) Yohani Kasaini amesema kufuatia agizo la Mkuu wa Mkoa watawaita wakandarasi wote haraka na kuwapatia maelekezo hayo pia watahakikisha wanawasimamia.
Kasaini amesema TANROADS kwa kushirkiana na Maafisa Kilimo na Mazingira wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi hususani wakulima kuacha kulima pembezoni mwa mito na kuharibu kingo za maji kama walivyofanya katika mto Zila Uliopo Wilayani Songwe na kupelekea kuharibika kwa barabara eneo la Nkanga.
Msimamizi wa Kampuni ya Sanka Building and Civil Engineering Lutufuyo Anyambilile Mwaikeke amesema wamepewa kazi ya kutengeneza barabara ya Chang’ombe-Patamela lakini kutokana na changamoto ya Mvua watafuata agizo la Mkuu wa Mkoa na kujikita katika eneo Nkanga ambalo limeharibika vibaya.
Mwaikeke ameongeza kuwa baadhi ya madereva wamekuwa wabishi kusikiliza maelekezo yao wanapo wakataza kuvuka barabara pindi maji yanapo jaa na hivyo kuleta usumbufu mara wanapokwama.
Naye Mkazi wa Chitete Wilaya ya Momba Thomas Siwiti amesema serikali ijitahidi kuboresha miundombinu ya barabara hususani maeneo ya madaraja kwakuwa yameonyesha kushindwa kuhimili wingi wa maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.