Home Mchanganyiko VIJANA WAFUNDISHWA UFUGAJI NYUKI KIBISHARA

VIJANA WAFUNDISHWA UFUGAJI NYUKI KIBISHARA

0

********************************

Chato

Vijana nchini wameshauriwa kujitokeza kuanziisha biashara ya ufugaji nyuki ili waongeze kipato na uhakika wa ajira Kijana Sambusa Jonathan wa kikundi Vijana Wafugaji Nyuki Kibiashara toka Singida amesema hayo wakati akitoa uzoefu na mafanikio katika kongamano la vijana katika kilimo wilayani Chato mkoani Geita leo (11.03.2020) ikiwa ni siku ya pili ya kongamano
hilo.

 

Jonathan amesema kikundi chao kinaundwa na vijana wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine wanaojishughulisha na ufugaji nyuki na kuchakata mazao ya nyuki.

 

Ametaja mazao ya nyuki kuwa ni uchakataji sumu ya nyuki ,asali,nta na mizinga ya kisasa ya kufugia nyuki.

 

Amewafahamisha vijana wanaoshiriki kongamano hilo kuwa soko la mazao ya nyuki lipo ndani na nje kutokana na umuhimu wake kiafya.

 

“Kikundi chetu kina mizinga 16,000 na kati yake 15,800 ina makundi ya nyuki”alisema Jonathan na kuongeza kuwa mizinga mmoja una uwezo wa kuzalisha lita moja kila baada ya miezi sita.

 

Endapo utahitaji kujua zaidi wasiliana nae: 0758787750
Akizungumza kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa SUGECO Revocatus Kimario amewapongeza vijana hao kwa ubunifu wao unaowasaidia kupata kipato na kuwataka
vijana wengine kwenda kujifunza Singida juu ya fursa ya manufaa ya ufugaji nyuki.

 

Kimario alisema vijana wa mikoa ya kanda ya ziwa wana nafasi nzuri kutokana na uwepo wa misitu na vyanzo vya maji kuanzisha biashara ya ufugaji nyuki.

 

“Hebu fikiria lita moja ya asali inauzwa shilingi 10,000 je mahindi au mpunga kilo moja inauzwa bei gani.Vijana tutafakari tunapotaka kuanzisha biashara” alisema Kimario.

 

Nae Revelian Ngaiza amesema Wizara ya kilimo na ile ya mifugo na Uvuvi inasisitiza vijana kuanzisha vikundi vya ufugaji ili kutumia uwepo wa mikopo ya vijana toka
Halmashauri kupata mitaji.

 

Kwa upande wake Maige Ikumbo mmiliki wa Ikumbo Enterprises ya Chato alitoa ushuhuda wa mafanikio aliyayapata katika biashara ya kuchakata ngozi za ng’ombe
kuzalisha bidhaa.

 

Alieleza kuwa ngozi zikichakatwa zinatoa manufaa mengi ikiwamo bidhaa bidhaa zinazopendwa na wateja kama viatu,kandamili,mikoba,mikanda na mabegi.

 

“ Sasa hivi nina uwezo wa kuchakata ngozi nne za ng’ombe kwa siku wakati bei ya ngozi moja kijijini ni shilingi 500 wakati nikimaliza uchakatazi napata hadi shilingi laki
tatu kwa ngozi moja “ alisema Maige.

 

Aliongeza kusema kuwa sasa amefanikiwa kuajili vijana wenzake saba katika ofosi yake iliyopo jingo la SIDO Chato na kuwa anakaribisha vijana wengi kwenda kujifunza
ushonaji na uchakatazi bidhaa za ngozi kwani kanada ya ziwa Victoria kuna malighafi ya kutosha ya ngozi.

 

Maige amewashauri vijana wenzake nchini kuwa na uthubutu kwani yeye aliacha kazi ya ufundi selemara na kuanzisha kiwanda kidogo cha kuchakata ngozi hali ilipelekea sasa kuwa na mtaji takribani milioni Ishirini.

 

“ Vijana wengi msiogope kuthubutu katika kuanzisha biashara yoyote muhimu tafuteni elimu na ujuzi “ alisema Maige.