Home Michezo MAANDALIZI MASHINDANO YA GOFU LUGALO OPEN YAPAMBA MOTO

MAANDALIZI MASHINDANO YA GOFU LUGALO OPEN YAPAMBA MOTO

0

***************************

Na Luteni  Selemani Semunyu

Maandalizi ya Mashindano ya TANAPA Lugalo Open yanaendelea vyema huku vilabu vyote Tanznaia vikithibitisha kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika  Ijumaa hadi Jumapili katika Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchji wa Tanzania Jijini Dar es salaam.

Akizungumzia Maandaalizi hayo Nahodha wa Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema Vilabu vilivyothibitisha ni Dar es Salaam Gymkana, Arusha Gymkhana, Morogoro Gymkhana, TPC Moshi, Kili Golf , Sea Criff ya Zanzibar na Wenyeji Lugalo Holf Club.

Alisema mwitikio umeendelea kuwa mkubwa na Kinachofanyika sasa ni Maandalizi ya Draw kwa ajili ya kuhakikisha  kila mchezaji anajua muda wake wa kucheza mapema ili waweze kushiriki kwa wakati ili kila mtu apate muda mzuri kucheza na kufurahia.

Kwa upande wake Afisa Tawala wa Klabu hiyo  Luteni Samwel Mosha amesema kwa Upande wa viwanja na shughuli zote za kiutawala zimekamilika pia zawadi kwa mujibu wa Wadhamini TANAPA zimeshanunuliwa na sasa kinachofuata ni  upangaji.

Akizungumzia kwa Upande wa Wachezaji wa Kulipwa Mchezaji wa Kulipwa Braison  Nyenza anayeratibu mashindano kwa wachezaji wa Kulipwa  alisema anachofanya ni  kupanga Draw kwa wachezaji wa Kulipwa na kutokana na Idadi ya wachezaji watacheza wachezaji wa Kulipwa Watano Watano.

“ Tutakuwa na Wachezaji wa Kulipwa wengi kutoka Vilabu Vyote hivyo katika kutimiza muda tutakuwa na idadi kulingana na Zawadi  ili kuhakikisha Mchezo unakuwa ni wa kuvutia na kuwa na ushindani mkubwa wakati wa mchezo” Alisema Braison.

 Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Michezo Utamaduni Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ambaye mbali na mambo mengine  atafunga Ofisi za Chama cha Gofu Tanzania na Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania TLGU ambazo  zitakuwepo Klabu ya Lugalo.