Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke pamoja na Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen
Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke akimuelezea jambo Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Katikati ni Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen.
Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen akimuuliza jambo Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro. Kushoto kwake ni Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke.
Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro pamoja na Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick wakifuatilia taarifa kuhusu mikakati ya kujikinga na kupambana na homa ya virusi vya corona
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick.
**************************************
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sarah Cooke, Balozi wa Norway nchini Mhe. Balozi Elisabeth Jacobsen pamoja na
Balozi wa Korea nchini Mhe. Balozi CHO tae-ick.
Dkt. Ndumbaro amekutana na mabalozi hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili masuala ya kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia pamoja na mikakati ya kujikinga na kupambana na homa ya virusi vya corona.
Pia, Mabalozi hao waliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika –SADC kwa maamuzi yake ya busara kupitia mawaziri wa Afya ya kuamua vikao vyote vinavyoendelea kufanyika kwa njia ya
mtandao yaani (Video Conference) ikiwa ni hatua mathubuti ya kukabiliana na maambukizi ya Ugonjwa huo.