Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa
SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ambao kwa sasa umeikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia
ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Kanali Wilbert Ibuge (wapili kutoka kushoto aliyevaa koti rangi Nyeusi) akiwa na wajumbe wengine wa SADC mara baada ya kuwasili katika mkutano na waandishi wa habari juu ya Mabadiliko ya mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakao fanyika kwa njia ya Mfumo wa Video kufuatia mripuko wa ugonjwa wa Corona (CODIV-19) ulioikumba nchi ya Afrika ya Kusini ambayo pia ni Nchi mwananchama wa Jumuiya ya SADC.
PICHA NA IDARA YA Habari-MAELEZO
***********************
NA EMMANUEL MBATILO
Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kilichopangwa kufanyika Machi 16 na 17 mwaka huu utafanyika kwa njia ya video kutokana na tishio la mlipuko wa virusi vya CORONA.
Amesema hayo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Kanali Wilbert Ibuge katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika Mkutano huo, Balozi Ibuge amesema kuwa utaratibu wa mkutano wa Baraza la Mawaziri unatarajiwa kufanyika Tanzania kama mwenyekiti wa Jumuiya hiyo utabadilika kwa kuufanya mkutano huo kwa njia ya video ambapo Mawaziri watafanya mkutano wakiwa katika nchi zao.
“Utaratibu huo wa mkutano kwa njia ya video umeridhiwa na Sekretarieti ya SADC pamoja na nchi mwenyekiti kwa kuwa unalenga kuondoa hatari ya kuenea kwa ugonjwa endapo mmoja kati ya washiriki atakuwa amepata maambukizi”. Amesema Balozi Ibuge.
Aidha, Balozi Ibuge amesema kuwa Tanzania kama Mwenyekiti wa SADC inatoa rai kwa serikali na wananchi wa Jumuiya ya SADC kuchukua hatua stahiki zinazopendekezwa na wataalam wa afya kujikinga na ugonjwa huo hatari ambao tayari umeshafika katika nchi mwanachama wa SADC, Afrika Kusini.
Pamoja na hayo Balozi Ibuge amesema kuwa Baraza la Mawaziri wa SADC litaendeshwa chini ya Mwenyekiti wake ambaye ni Waziri wa Mambo ya NJe na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.Palamagamba Kabudi na kushirikisha Mwaziri wanaoshughulikia Mambo ya Nje, Viwanda, Biashara, Fedha na Mipango kutoka nchi wanachama wa SADC.
Vilevile Miongoni mwa ajenda muhimu zilizopangwa kujadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na utekelezaji wa kauli mbiu ya mwaka huu ya Jumuiya hiyo isemayo “Mazingira wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuiya ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC”.