Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu (mwenye kofia
nyekundu) akishiriki katika zoez la kusafisha fukwe za bahari katika eneo la Salander Bridge ikiwa ni
mwaliko wa kikundi cha Utunzaji Mazingira cha Save the coast
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiwa katika picha
ya pamoja na Wananchi waliojitokeza katika zoezi la usafishaji wa fukwe za bahari maeneo ya Salander
Bridge jijini Dar es Salaam.
****************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu ameawagiza Wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni kuhakikisha fukwe zote zilizopo katika Manispaa zao zinasafishwa na kufanyiwa usafi kila mara na kukusanya uchafu wote uliokusanywa katika maeneo ya fukwe.
Ameyasema hayo wakati aliposhiriki usafi wa kusafisha fukwe za bahari eneo la Salander Bridge
jijini Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa anawashukuru sana kikundi cha utunzaji wa mazingira cha Save the Coast kwa kumualika kujumuika pamoja nao kusafisha fukwe na pia kawapongeza kwa moyo na ari yao kubwa ya kusafisha fukwe za Bahari na kuziacha katika mazingira ya usafi.
“Ninawapongeza wote lakini tushirikiane katika, kutunza mazingira ili kuwaachia kizazi kijacho mazingira safai na salama” alisema Zungu.
Ziara hiyo ya Mheshimiwa Zungu kusafisha fukwe za bahari za Ocean ni mwaliko alioupata kutoka kwa
kikundi cha mazingira cha Save the Coast ikiwa ni utaratibu wa mara kwa mara kufanya usafi katika
fukwe mbalimbalimbali katika jiji la Dar es Salaam.