Home Mchanganyiko ASKARI KUJENGEWA UWEZO WA KIMEDANI PORI LA MKOMAZI

ASKARI KUJENGEWA UWEZO WA KIMEDANI PORI LA MKOMAZI

0

**************************

08/03/2020 MKOMAZI, TANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amefanya ziara ya ukaguzi katika eneo la uwanja wa mbinu za medani lililopo Mkomazi mkoani Tanga eneo ambalo ni mahusus kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa kimedani askari wa Jeshi hilo katika kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.

 

IGP Sirro pia amezungumza na baadhi ya wananchi wa eneo la Manga wilaya ya Handeni mkoani humo na kuwataka kuendelea kuimarisha amani ya nchi na
kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

 

IGP Sirro amemaliza ziara yake ya kikazi kwa kufanya ukaguzi kwa kutembelea mikoa mitatu ikiwemo Manyara, Arusha na Kilimanjaro.