Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wanakijiji wa Isoliwaya (hawapo pichani) wilayani Kilolo, Iringa kabla hajazindua mnara wa mawasiliano. Wa kwanza kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba na wa pili kushoto ni Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa na Vodacom kwa ruzuku ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kijiji cha Idodi mkoani Iringa. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba na kushoto kwake ni Mkuu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Vodacom, Ezekiel Nungwi
Mkazi wa Kijiji cha Isoliwaya wilayani Kilolo mkoani Iringa, Vitolina Mbweli akipokea simu mpya ya mkononi kutoka kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye alipofika kuzindua mnara wa mawasiliano kijijini hapo. Simu hiyo imenunuliwa na Mbunge wao wa Kilolo, Venance Mwamoto (wa kwanza kushoto)
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba akizunguza na wanakijiji wa Isoliwaya wilayani Kilolo, Iringa (hawapo pichani) kabla ya Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kulia) kuzindua mnara wa mawasiliano kijijini humo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Hapiness Seneda (wa pili kushoto) alipofika ofisini kwake kabla ya ziara ya kuzindua minara ya mawasiliano mkoani humo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Dkt. Joseph Kilongola na wa tatu kulia ni Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo, Justina Mashiba.
**************************
Na Prisca Ulomi, WUUM, Iringa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kuwapatia
wananchi huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu ikiwemo huduma ya data na sauti katika maeneo mbali mbali nchi nzima ambapo inatoa huduma zake.
Pongezi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiwa ziarani mkoani Iringa kuzindua minara ya mawasiliano iliyojengwa na TTCL, Vodacom na Halotel kwa kutumia ruzuku ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotolewa kwa kampuni za simu za mkononi kujenga
minara hiyo kwenye maeneo ya vijijini na siyo na mvuto wa kibiashara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
Nditiye amefanya uzinduzi wa minara ya mawasiliano ya TTCL mkoani humo kwenye kata ya Kihesa, minara ya Vodacom kwenye kata ya Idodi na ya Halotel kwenye kata ya Ihimbo mkoani humo ambapo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni moja ambazo zimetolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kampuni hizo
za simu ili kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi zaidi ya laki moja kwenye kata hizo na maeneo ya jirani mkoani humo.
Alisema kuwa TTCL imedhihirisha kuwa mnaweza tangu Serikali ilipofanya maamuzi ya kuwafanya kuwa Shirika la Mawasiliano Tanzania linalomilikiwa na Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia mia moja baada ya kuibadilisha kutoka kuwa Kampuni ya Simu Tanzania baada ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na
Dkt. John Pombe Magufuli kuingia madarakani.
“Kila mnakopatikana mawasiliano ni mazuri, ni ya uhakika na hakuna kukatakata, mnaweka bei ambazo mtu akipiga simu anajiuliza mnatoa huduma bure au la! Na mwisho wa siku faida inayopatikana mnarudi nyumbani na kusema baba(Serikali) faida hii tumepata, endeleeni kuchapa kazi kwa kuwa ninyi ndio watanzania wenyewe, fanyeni kazi na watanzania waone mnafanya kazi kwa kuwapatia watanzania huduma za mawasiliano, kumbe mnaweza na mnaweza sana, hakikisheni kila mahali vocha zipo na laini zenu zipo” amesisitiza Nditiye.
Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema kuwa wamepeleka mawasiliano kwenye kata 956 maeneo mbali mbali nchini
ambapo hadi sasa ujenzi wa minara ya mawasiliano kwenye kata 565 umekamilika na wananchi wanapata huduma za mawasiliano na ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu watanzania wapatao milioni 8 waishio pembezoni na maeneo ya vijijini watapata huduma za mawasiliano.
Mbunge wa Iringa Mjini mkoani humo, Peter Msigwa ameipongeza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma za mawasiliano kwa kuwa siku hizi uchumi hautumii misuli bali akili ambapo sasa akili ni Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo inatumika kutengeneza mabilioni ya fedha ambapo ni tofauti na zamani watu walikuwa wanatumia nguvu mfano kulima eneo
kubwa.
Vile vile Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto akizungumza kwa niaba ya wananchi wake ameishukuru Serikali kwa kujenga minara ya mawasiliano kwenye maeneo yao kwa kuwa sasa mawasiliano ni maendeleo na amewataka wananchi kusema ukweli na kueleza bayana maendeleo yanayoletwa na Serikali na kuwataka walinde miundombinu ya mawasiliano kwa kuwa ni mali yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanakiji cha Isoliwaya wilayani Kilolo mkoani Iringa, Vitolina Mbweli ameishukuru Serikali kwa kujenga mnara wa mawasiliano kijiji humo kwa kuwa sasa mawasiliano yanapatikana na amepatiwa simu mpya ya mkononi na Mwamoto ambapo hakutegemea kumiliki simu ambayo itamwezesha kuwasiliana