Msimamizi wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga akitoa maelezo mafupi kwa wanawake kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) hawapo pichani leo katika kutoa mkono faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 08 Machi, 2020.
Baadhi ya wanawake kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI), wakiwa wamebeba moja ya mahitaji katika kutoa mkono faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma leo katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 08 Machi, 2020.
Wanawake kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa mkono faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma katika kuelekea leo maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 08 Machi, 2020.
…………………………………………………………………………………….
Na. Majid Abdulkarim
Katika kuelekea Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika kesho Machi 08, 2020 wanawake kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo wametoa mkono wa faraja kwa Kituo cha kulelea Watoto yatima cha Nyumba ya Matumaini Miyuji kilichopo Jijini Dodoma.
Wanawake hao wamesema kuwa mkono huo wafaraja ni kuwafariji Watoto hao kujihisi kuwa ni sehemu ya jamii ya watanzania na kuwafanya kuwa na amani kwani hakuna hajuaye kesho yake.
Pia wametoa wito kwa Watoto hao kuendelea kuwa na nidhamu na kufanya vizuri katika masomo yao na kutaka wajisikie kuwa wako pamoja nao nan do maana kuelekea siku ya wanawake Duniani tuko pamoja kuonyesha upendo wa mama kwa mtoto.
Wakati huohuo msimamizi wa kituo hicho Sista Anitha Kasanga amebainisha changamoto katika kituo hicho kuwa ni uhaba wa vitanda vya kulalia Watoto hao na bima za afya kwa ajili ya kuwatibia Watoto hao wanapo ugua.
“Muda wowote tunapokea Watoto wa itikadi yoyote kwani lengo letu ni kuwalea na kuwahudumia Watoto wote bila kubagua, hivyo tunaomba jamii na wadau mbalimbali waendelee kujitokeza kwani umoja ni nguvu”,amesema Sista Kasanga
Sista Kasanga ameeleza kuwa kituo hicho kwa sasa kina Watoto 64 kutokana baadhi ya Watoto wako katika shule za bweni.
Naye mmoja wa Watoto wanaolelewa katika kituo hicho (jina kimeifadhiwa) ametoa neno la shukrani kwa kusema Mungu awabariki sana wanawake kutoka TAMISEMI pamoja na watumishi wote ambao hawakuweza kufika.
“Katika kuelekea siku ya wanawake duniani tumefarijika kwa upendo wenu wa kutukumbuka kwa mahitaji muhimu mlotuletea na Mungu awazidishie mlipo toa “, ameshukuru mtoto huyo.
Kila mwaka 8 Machi wanawake duniani kote huadhimisha siku ya wanawake duniani, ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Simiyu na kwa hapa Jijini Dodoma yatafanyika Shule ya Msingi Mkonze.