Home Mchanganyiko TET YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA OCEAN ROAD.

TET YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA OCEAN ROAD.

0

***************************

Wanawake wa TET Leo wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa wa saratani wanaopata matibabu katika Taasisi ya saratani ya ocean road iliyopo Dar es salaam.

Alikabidhiwa msaada huo kwa niaba ya Wanawake wengine wa TET, Mwenyekiti wa Wanawake Bi. Agusta Kayombo amesema msaada waliotoa ni sehemu ya jukumu la TET katika kujali jamii.

‘Hiki tunachotoa kwa wagonjwa kinaweza kua ni kidogo lakini ni sehemu ya jukumu la TET katika kujali jamii.Ambapo Leo katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani tumekabidhi vifaa Tiba,Kanga, Sabuni, Mafuta ya kupaka, miswaki na dawa za meno.

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt.Aneth Komba amewaelekeza Wanawake wa TET kujiamini katika kazi zao wasikubali kunyanyaswa kijinsia,ikiwa yeye ni kiongozi Mwanamke atasimama imara katika kutetea na kuhakikisha Haki na usawa wa Mwanamke.