Home Michezo MKWIRU NA USHIRIKA WAKE ONE TEAM KUIPAISHA TIMU YA MWAMBISI SEK KUPATA...

MKWIRU NA USHIRIKA WAKE ONE TEAM KUIPAISHA TIMU YA MWAMBISI SEK KUPATA UZOEFU GERMAN

0
…………………………………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,Pwani
WADAU wa michezo kutoka German One Team kwa ushirika na Ibrahim Mkwiru ,wameeleza ndoto yao ya kuchukua timu ya mpira wa miguu ya wanafunzi wa kike, katika shule ya sekondari ya Mwambisi kwenda nchini Ujeruman kuchota uzoefu na timu nyingine za shule za sekondari nchini humo ili kuwa na uzoefu.
Aidha ushirika huo,umeeleza mpira wa miguu sio kwa ajili ya watoto wa kiume pekee hivyo watoto wa kike wanapaswa kujiandaa kuucheza kuanzia mashuleni ili kuweza kuchukuliwa na timu kubwa za wanawake .
Akizungumza wakati wa bonanza waliloliandaa shuleni hapo na kushirikisha timu za mtaani Tanita,sekondari ya westage na sekondari Mwambisi,ambazo wanazifadhili kuzipa vifaa mbalimbali za michezo,Mkwiru alieleza ,timu ya wasichana ya mpira wa miguu Mwambisi na timu ya mpira wa mikono ipo juu hivyo endapo itapewa uzoefu na kufanyiwa mazoezi makubwa itapiga hatua na kuopoa vijana wachezaji chipukizi kuingia kwenye timu kubwa nchini.
Hata hivyo ,alibainisha tangu mwaka 2015 ameshatoa kontena la vifaa vya michezo ikiwemo mipira 50 na kuwezesha timu mbalimbali kutatua changamoto ya vifaa ambapo pia amekabidhi mipira mitano na jezi katika timu zilizoshiriki kwenye bonanza hilo .
Nae mdau wa mpira kutoka German Caroline Carolin Smarzorch,alifafanua, nchi inayotaka kuendelea kisoka lazima wajenge uwezo kwa timu kuanzia mashuleni na mitaani ili kupata timu za vijana wenye uzoefu mkubwa .
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Mwambisi, Joseph Simba alitaja changamoto ya baadhi ya ,wazazi wamekuwa wakiwakataza watoto wao wa kike wasishiriki kwenye mpira wa miguu kwani kimaadili katika uvaaji wanakuwa wanavaa pensi na changamoto nyingine ni uwanja bora kwa ajili ya mpira wa kikapu na pete,jezi na mipira.
Pamoja na hilo mwl simba anasema ,jamii inapaswa ijue kwamba kuna watoto ambao hawapo vizuri kitaaluma lakini kwenye michezo wana vipaji .
“Wazazi wanatakiwa kujua nini mtoto anataka,anapenda,mtoto anatakiwa asome lakini kama anapenda na michezo asikatazwe kabisa afanye vyote kwa wakati mmoja maana hajui atoatokea wapi kimaisha”alisisitiza Simba.
Mwanafunzi wa kidato cha pili Zainab Sultan amesema ni captain wa timu ya kike ya miguu shuleni hapo na anatarajia kuwa kama Gaucho.
Katika mchezo huo ulioshirikisha timu mbalimbali, timu ya mpira wa miguu ya wanafunzi wa kike Mwambisi iliibuka kidedea kwa kuifuga sekondari ya westage ,na mpira wa mikono mwambisi iliibamiza westage kwa mabao 20 kwa moja.
Shule ya sek mwambisi ni shule inayofanya vizuri kitaaluma na inaogopewa kwa michezo na timu za mitaani na shule jirani endapo itapata support itapiga hatua kuanzia wilaya,mkoa na taifa.