Home Mchanganyiko MKOA WA DODOMA KUANDAA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU

MKOA WA DODOMA KUANDAA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza  tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa

Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao ofisini kwake  kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza  tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa

Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Maria Lyimo,akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza  tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa

………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma.
Mkoa wa Dodoma unatarajia kuandaa kongamano la Wadau wa Elimu kuanzia
tarehe 21-22 mwezi huu 2020.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema lengo  la kongamano hilo ni kwa ajili ya   kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu Mkoani Dodoma hali ambayo husababisha kiwango cha elimu kuwa cha chini mkoani hapa licha ya kuwa ni makao makuu ya nchi.

Dkt.Mahenge ametaja baadhi ya viashiria vinavyosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika mkoa wa Dodoma ni pamoja na umbali mrefu wa shule  ,ufuatiliaji hafifu pamoja na mwamko mdogo wa wazazi juu ya masuala ya elimu pamoja na miundombinu isiyokuwa toshelezi.

Hivyo kongamano hilo  litakutanisha wadau ili kuchambua mikakati  za kuinua kiwango cha elimu mkoani Dodoma ambapo kutakuwa na shughuli  kuu mbalimbali.

Aidha amesema kuwa kutakuwa na uzindua wa kampeni endelevu ya ushiriki wa jamii katika uchangiaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule ,kufanya tathmini ya hali ya maono ya wananchi ushiriki maendeleo ya elimu ,kubainisha masuala ya kiupambele katika kuboresha sekta ya elimu pamoja  kuamsha hamasa kwa jamii katika suala la elimu kwa kutoa tuzo mbalimbali kwa  walioonesha juhudi  katika suala la elimu.

Naye Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Maria Lyimo amesema jamii inatakiwa kuelewa
dhana ya  sera ya elimu ya Msingi bila malipo kwani mzazi ana jukumu la kumnunulia mtoto wake mahitaji ya Msingi ya shuleni.

Kaulimbiu katika kongamano hilo ni “kuinua Kiwango cha Elimu katika Mkoa wa Dodoma huku Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa .