Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge,(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao ofisini kwake kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa
Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Maria Lyimo,akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kongamano la wadau wa elimu litakaloanza tarehe 21 hadi 22 mwezi huu,2020 na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma.
Mkoa wa Dodoma unatarajia kuandaa kongamano la Wadau wa Elimu kuanzia
tarehe 21-22 mwezi huu 2020.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo jijini Dodoma,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge amesema lengo la kongamano hilo ni kwa ajili ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya Elimu Mkoani Dodoma hali ambayo husababisha kiwango cha elimu kuwa cha chini mkoani hapa licha ya kuwa ni makao makuu ya nchi.
Dkt.Mahenge ametaja baadhi ya viashiria vinavyosababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika mkoa wa Dodoma ni pamoja na umbali mrefu wa shule ,ufuatiliaji hafifu pamoja na mwamko mdogo wa wazazi juu ya masuala ya elimu pamoja na miundombinu isiyokuwa toshelezi.
Hivyo kongamano hilo litakutanisha wadau ili kuchambua mikakati za kuinua kiwango cha elimu mkoani Dodoma ambapo kutakuwa na shughuli kuu mbalimbali.
Aidha amesema kuwa kutakuwa na uzindua wa kampeni endelevu ya ushiriki wa jamii katika uchangiaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule ,kufanya tathmini ya hali ya maono ya wananchi ushiriki maendeleo ya elimu ,kubainisha masuala ya kiupambele katika kuboresha sekta ya elimu pamoja kuamsha hamasa kwa jamii katika suala la elimu kwa kutoa tuzo mbalimbali kwa walioonesha juhudi katika suala la elimu.
Naye Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Maria Lyimo amesema jamii inatakiwa kuelewa
dhana ya sera ya elimu ya Msingi bila malipo kwani mzazi ana jukumu la kumnunulia mtoto wake mahitaji ya Msingi ya shuleni.
Kaulimbiu katika kongamano hilo ni “kuinua Kiwango cha Elimu katika Mkoa wa Dodoma huku Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa .