Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba (katikati) akiwa na viongozi wengine wa Mamlaka hiyo, wakati akizungumza leo Machi 5 mwaka 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na waandishi waandamizi.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini wakati wa kikao kazi.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakiwa makini kufuatilia mada zilizokuwa zinatolewa wakati wa kikao kazi kati yao na maofisa wa TCRA wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba.
Mkurugenzi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Connie Francis akielezea kwa kina namna ambavyo TCRA inafanya shughuli zake zikiwemo za kusimamiwa wadau wao.
******************************
NA MWANDISHI WETU
KWA mara ya kwanza hapa nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itatoa Tuzo kwa Makampuni mbalimbali yanayotoa Huduma Bora za Mawasiliano.
Akizungumza leo Machi 5,2020 wakati wa kikao kazi na wahariri na waandishi wa habari waandamizi wa vyombo vya habari nchini, kwenye makao makuu ya TCRA jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James M. Kilaba amesema lengo kuu la Tuzo hii, ni kutambua na kutunza Kampuni zitakazo chaguliwa kwa kutoa Huduma Bora. Pia kuhamashisha Ubunifu katika utoaji wa Huduma za Mawasiliano.
Makampuni yote yaliyopewa leseni na TCRA ya kutoa huduma ya Mawasiliano yanawajibika kuwasilisha maombi ya kushiriki kabla ya Tarehe 15 Machi, 2020.
Alisema uteuzi utaanza tarehe 16 hadi 31 Machi, 2020 na uteuzi wa waliokidhi vigezo vya kushiriki.
Tarehe 1 hadi 30 Aprili 2020- Wananchi watapata fursa ya kupiga kura kuchagua Kampuni ipi ina Huduma Bora ipi yenye Ubunifu inayo Faidisha Wananchi.
Alisema Tarehe 15 Mei, 2020 Sherehe kubwa ya Kutoa Tuzo kwa Watoa Huduma Bora itafanyika Mlimani City Jijini Dar Es Salaam na Kuhudhuriwa na Viongozi wa Juu wa Nchi, pamoja na Wakuu wa Tasisi za Mawasiliano wa Umoja wa MaTaifa (UN) Wanao simamia Mawasiliano Ulimwenguni, ikiwemo Tasisi ya Mawasiliano Duniani ITU- Geneva, Umoja wa Posta Duniani ( UPU), Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Tasisi nyinginezo.
Mhandisi Kilaba Alisema Tuzo 17 zitatolewa kwa Makampuni 15, ya huduma za aina mbali mbali.
Aliyataja Makampuni hayo kuwa ni pamoja na, Watoa Huduma za Utangazaji, Radio na Televisheni, Kampuni Bora ya Radio na Televisheni Mtandaoni, Kampuni yenye Huduma Bora ya Simu za Mkononi, Kampuni Bora ya Huduma za Posta na Usafirishaji wa Vifurushi na Vipeto, Kampuni Bora ya Huduma za Intanet na, Kampuni Bora ya Wasambazaji wa Maudhui ( Multiplex Operators)
Zingine ni Blog Bora, Kampuni Bora ya Utoaji wa Huduma za Intanent na Kampuni nyingine zote zenye leseni ya TCRA.
” TCRA imedhamiria kuongeza Ustawi wa Wananchi wa Tanzania kwa Kupitia Huduma Bora za TEHAMA zenye Ubunifu zinazo Faidisha Jamii” amesema Mhandisi Kilaba.
Zaidi wa Wahariri 50 wa Vyombo vya Habari mbalimbali hapa nchini wamehudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika makao makuu ya TCRA, Mawasiliano Towers, jijini Dar Es Salaam, Tarehe 5/03/2020.