Home Burudani KOFFI OLOMIDE KUBURUDISHA SHEREHE ZA MIAKA ISHIRINI YA CLOUDS MEDIA MLIMANI CITY

KOFFI OLOMIDE KUBURUDISHA SHEREHE ZA MIAKA ISHIRINI YA CLOUDS MEDIA MLIMANI CITY

0

********************************

Na Magreth Mbinga

Mwanamuziki Koffi Olomide kutoka Congo DRC ambaye anafanya muziki aina ya Bolingo amewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuburudisha baada ya kupata mualiko kutoka Clouds Media ambao wanasherehekea miaka ishirini ya burudani tangu kuanzishwa kwake.

Kofi Olomide amezungumza na waandishi wa habari katika Hoteli Serena jijini Dar es salaam leo baada ya kuwasili nchini. “Moyo wangu umefurahi kufika nchini Tanzania nasema asante kwa wote walioandaa shughuli hii” .Aliasema Olomide

Pia amesema watu wote wafike siku ya kesho Mlimani City bila kukosa kwaajili ya kupata burudani na amewataka wapenzi wa burudani kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wafike bila kukosa ili wafurahi kwa pamoja katika usiku huo wa burudani

Tamasha hilo la kufungua mwaka limeandaliwa na clouds media katika lush where kea miaka shirini ya kutoa burudani .

Olomide amemalizia kwa kuwakaribisha wapenzi wa muziki hasa aina ya bolingo wafike bila kukosa wapate burudani ya kutosha kutoka kwake na bendi yake.