Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir Saleh akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinavyoendelea kiwandani hapo.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakielekea katika eneo la uzalishaji wa Trasfoma wakati walipotembelea kiwanda cha Tanalec Limited cha jijini Arusha.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea na kazi ya uzalishaji wa Trasfoma.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir Saleh akiwapa maelezo waandishi wa habari namna uzalishaji wa Trasfoma unavyoendelea walipotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinavyoendelea.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir Saleh akiwaonesha waandishi wa habari baadhi ya Transfoma ambazo ziko katika hatua mbalimbali za utengenezaji wakati waliotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli za uzalishaji zinavyoendelea.
…………………………………………………..
Soko la Trasfoma kwa Tanzania nikubwa sana ukilinganisha na kipindi kiingine ambapo kwa mwaka uliopita tumeuza Transfoma 8000 huku mradi wa umene vijijini peke yake wakichukua Transfoma 300.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Transfoma cha Tanalec Limited cha jijini Arusha Bw. Zahir Saleh ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda hicho ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinavyoendelea kiwandani hapo.
Bw. Zahir amesema soko la Tanzania ni kubwa na wao wanakidhi haja ya soko kwa sababu uzalishaji wa Transfoma na vifaa mbalimbali unaenda vizuri na kwa kiwango cha hali ya juu.
“Nalipongeza shirika la umeme nchini TANESCO kwa kudhibiti tatizo la kukatikakatika kwa umeme na kuzalisha umeme wa kiwango kizuri na wakutosha, hili limetufanya kuendelea vizuri na uzaishaji wa bidhaa kiwandani hapa”.
Umeme kwa sasa kukatika imekuwa ni historia inaweza kupita hata miezi mitano ukakatika mara moja na baada ya muda mfupi unarudi kwa kweli kwa hili nawapongeza TANESCO” Amesema Bw. Zahir Saleh.
Amesema kwa sasa wanayo masoko mengine katika nchi nyingi za Afrika kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Ethiopia na nyingine.
Amesema lengo kiwanda hicho ni kuzifikia nchi nyingi za Afrika ili kupanua soko zaidi huku akitolea mfano wa Kenya ambayo imewapa tenda ya Dola Milioni sita ili kuwauzia Transfoma.