…………………………………………………………………………….
Viingilio vya mchezo wa raundi ya pili ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga vyawekwa hadharani.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limetangaza viingilio ni shiling 7000 kwa viti vya mzunguko, Viti vya Machungwa vikikaliwa kwa shilling 1000, VIP B na C itakuwa ni 15000 na VIP A kwa shiliing 30,000.
Taarifa hiyo iliyotolewa na TFF mapema leo, imeeleza kuwa mchezo huo utapigwa majira ya sa 11 jioni katiia Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa pande zote, itachezwa siku ya Jumapili ya Machi 08, huku kila upande ukijinasibu kuibuka kidedea.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa January 04, Timu hizo zilitoka sare ya goli 2-2 Simba wakitangulia kufunga magoli yaliyofungwa na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Rwanda Meddie Kagere na Deo Kanda ambapo Yanga walisawazisha kupitia kwa Kiungo Mapinduzi Balama na Mohamed Issa ‘Banka’.
Simba kwa sasa wanaongoza msimamo wa ligi Kuu wakiwa na alama 65 na siku ya Jumatano atashuka dimbani kuvaana na vijana wa Chamazi Azam Fc katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga nao wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 45, watacheza kesho dhidi ya Mbao Fc ya Jijini Mwanza ambapo michezo yote hiyo itapigwa majira ya sa 1 usiku.
Tambo za mashabiki wa pande zote mbili zinaendelea kila mmoja akiamini anaenda kuondoka na alama tatu muhimu.