Katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega akipongeza mwenyekiti wa bodi ya shule ya Mrisho Gambo Mhandisi Dkt.Richard Masika baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi
……………………………………..
Katibu tawala mkoa wa Arusha Richard Kwitega amezindua bodi ya shule ya sekondari ya Mrisho Gambo iliyopo katika kata ya Olasiti Jijini Arusha.
Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo kwa niaba ya mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,Kwitega aliitaka bodi hiyo kuhakikisha kuwa inasimamia ubora wa elimu na kuhakikisha inafanya vizuri na kuwa ya mfano.
Pia alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo ulitokana na kuongezeka kwa ufaulu katika mkoa wa Arusha hivyo kulazimika kutafuta namna ya kutatua changamoto hiyo ya wingi wa Wanafunzi.
Aidha alisema kuwa Serikali ya mkoa wa Arusha itaendelea kutoa ushirikiano kwa bodi hiyo ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi unaotakikana.
Kwa Upande wake Mhandisi dkt.Richard Masika ambaye alichaguliwa na wajumbe wenzake wa bodi kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo alisema kuwa bodi hiyo itafanya kila linalowezekana katika kuhakikisha kuwa elimu na mafunzo yanayotolewa shuleni hapo ni ya ubora wa hali ya juu.
Mhandisi Masika alisema kuwa bodi hiyo imepanga kuhakikisha kuwa shule hiyo inakuwa ya kwanza kimkoa na kitaifa huku swala la nidhamu litakuwaa ni la Hali ya juu.
Nae makamu mwenyekiti wa bodi hiyo ya shule Faraja Nyalandu alimshukuru katibu tawala kwa kuzindua bodi hiyo na mkuu wa mkoa wa arusha kwa uteuzi na kuahidi kuwa watashirikiana na walimu wa shule hiyo katika kuhakikisha kuwa kiwango Cha elimu katika shule hiyo kinakuwa Juu.
Faraja alisema swala la Nidhamu ni kipaumbele Cha kwanza Cha Wanafunzi ili kupata matokea Bora Zaidi.
Bodi hiyo inaundwa na wajumbe nane ambapo kuzinduliwa kwake ni kuashiria kuwa kazi imeanza rasmi.
Mkoa wa Arusha ni mkoa ambao umekuwa ukifanya vyema katika ufaulu hapa nchini Hali ambayo imekuwa ikiiupa uongozi wa mkoa changamoto ya kuhakikisha kuwa Wanafunzi wote wanaofaulu wanaendelea na masomo.