Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakisikiliza maelekezo kabla ya kufanya uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Antelmas Tarimo (aliyesimama) akitoa sifa za wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kabla ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza hilo.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Deogratias Yinza akiongoza kikao cha uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Msimamizi wa uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Neema Dickson (kulia) akisimamia zoezi la kuhesabu kura.
Msimamizi wa uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Neema Dickson (kulia) akisimamia zoezi la kuhesabu kura.
****************************
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara ya Katiba na Sheria Ndg. Deogratias Yinza awataka
wajumbe waliochaguliwa kuwawakilisha wenzao kwenye baraza la wafanyakazi kuhakikisha wanawakilisha vyema mawazo ya wenzao waliowachagua.
Hayo ameyasema kwenye zoezi la uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara hiyo baada ya wajumbe wa awali kumaliza muda wao mwishoni mwa mwaka jana.
“Wawakilishi mliochaguliwa kuwawakilisha wenzenu kwenye baraza la wafanyakazi mhakikishe mnawakilisha vyema mawazo ya waliowachagua” alisema.
Aidha, Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Bw. Antelmas Tarimo alitaja sifa za mjumbe wa baraza ikiwmo mtu anayejitambua, anayejitoa na mchapakazi, pia awe anajua baadhi ya mambo ya kisheria na utumishi ili kumwezesha kuhoji vizuri mambo muhimu mfano haki za watumishi.
Aliongeza, wajumbe wazuri wanaotoa mawazo ya kusaidia taasisi ni muhimu kwenye baraza na sio kuangalia urafiki ili kuboresha maslahi na utendaji wa taasisi.
“Usichague mtu sababu ni rafiki au mmezoeana”, alisema Tarimo.
Naye Afisa kazi Mkoa wa Dodoma Bi. Neema Dickson ambaye ni msimamizi mkuu wa uchaguzio huo alisema waliochaguliwa washiriki ipasavyo kuwawakilisha wenzao ili kutatua changamoto zinazo wakabili na kuwakilisha mawazo yao vyema kwa viongozi wa baraza.
Katika uchaguzi huo kila Idara na Kitengo ilichagua mjumbe ambaye ana jukumu la kuwasilisha mawazo
na maoni yake pamoja na ya wenzake katika kikao cha baraza la wafanyakazi kinachofanyika kila mwaka.