Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Anne Makinda akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Jijini Dodoma leo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifafanua jambo wakati wa Kongamano la uzinduzi wa siku ya Wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wakimsikiliza mgeni Rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda lililofanyika leo jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea hatua za utekelezaji wa maazimio ya Ulingo wa Beijing katika Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dodoma
Waziri Mstaafu na Spika wa kwanza wa Bunge la Afrika Getrude Mongella akizungumza na washiriki wa Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani lililofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya wanafunzi walioshiriki Kongamano la uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani wakimsikiliza mgeni Rasmi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda lililofanyika leo jijini Dodoma.
Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania Anne Makinda,akifunguzi rasmi Kongamano kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya wanawake Duniani yatakayofanyika Mkoani Simiyu kwa Kauli mbiu KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA BAADAYE leo jijini Dodoma
………………………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Spika msaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda amewataka wanawake nchini kuacha uoga katika wakati wa mapambano ya kutafuta fursa mbalimbali za kielimu, uchumi na siasa vinginevyo masuala ya usawa wa kijinsia itabaki kuwa ndoto.
Makinda amesema hayo jijini DODOMA katika Kongamano la uzinduzi wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambalo pamoja na mambo mengine limejadili utekelezaji wa maazimio ya ulingo wa Beijing yaliyowekwa miaka 25 iliyopita.
Amesema wanawake nchini Tanzania ni zaidi ya asilimia 51 ya wananchi wote hivyo kundi hili lina uwezo kufikia maamuzi yenye tija kwa wanawake lakini tatizo kubwa ni woga wa kuthubutu ilhali uwezo wanao.
“Wanawake acheni uoga na unyonge maana wanawake ambao ni wawakilishi wa majimbo wameendelea kuaminika na kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa amesema.
Ameongeza kuwa, jitihada zinaonekana ingawa zinasuasua sana hasa kwenye mambo ya siasa.
Hatuwezi kusema tuna usawa wa kijinsia wakati bado hatujaweza kuchaguliwa na watu. Kama isingekuwa kipengele cha viti maalum, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lingekuwa na wanawake asilimia 6 tu, idadi ambayo ni ndogo sana”
Ameongeza kuwa asilimia 30 ya wabunge wa viti maalum na wale wa kuteuliwa haina mantiki katika kuelekea usawa wa kijinsia.
Amewahimiza wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi hasa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema mchango wa viongozi wanawake wakiwemo wastaafu umeleta mabadiliko makubwa katika kuelekea maendeleo jumuishi.
Waziri Mwalimu amemtaja Mama Makinda kuwa kuwa kioo kwake wakati wa kutekeleza majukumu yake katika Wizara huko akiwapongeza wanawake walioshiriki katika harakati za kuelekea ukombozi wa mwanamke maarufu kama Mkutano wa BEIJING.
Akizungumza kwa niaba ya Mtandao wa wabunge Magaret sitta amesema kuwa hawawezi kupata viongozi wanawake wengi zaidi kama watoto wa kike hawasomi huku mwakilishi wa mtandao wa jinsia Tanzania[TGNP]Asien Muro akisema katika kongamano hilo ni vyema kutumia kama fursa kwa kuangalia changamoto zinazowakabili wanawake .
Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Mhandisi Stella Manyanya amesema akina mama wana mchango mkubwa katika ujenzi wa viwanda na biashara ambapo 80% ya wafanyakazi katika uzalishaji wa viwanda vya nguo na korosho ni wanawake.
Naye Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amewataka akina mama kuchangamkia fursa za elimu katika Nyanja za sayansi na teknolojia na kuhakikisha watoto wa kike wanapelekwa shule huku Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Augustine Mahiga akibainisha kuwa Wizara inaendelea kuhakikisha kuwa sheria zinampa nafasi zaidi pamoja na kumlinda mwanamke.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiwasilisha utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Beijing amesema mambo mengi yamefanyika ikiwemo kuwezesha wanawake kiuchumi kupitia mifuko ya uwezeshwaji kiuchumi.
Dkt. Jingu amesema kwa kipindi cha miaka minne, zaidi ya shilingi bilioni 39 zimetolewa kwa wanawake zaidi ya laki 8 kupitia asilimia 10 ya fedha za ndani za Halmashauri na shilingi bilioni 2 zimetolewa kwa zaidi ya wanawake elfu 3 kupitia dirisha la wanawake la Benki ya Posta Tanzania mwezi Agosti 2018 hadi Machi 2019.
Ameongeza pia kuwa, umiliki wa ardhi umeongezeka kwa wanawake kutoka asilimia 6 mwaka 2014 hadi 16 mwaka 2017 pamoja na ushiriki wa wanawake katika maonesho ya Biashara ya kimataifa kutoka 1183 mwaka 2017 hadi 13016 mwezi Machi mwaka 2019.
Kongamano hilo la siku moja limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa afya na wanafunzi kutoka shule za Sekondari zilizopo mkoani Dodoma.
Kusanyiko hilo ni ufunguzi rasmi kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya wanawake Duniani yatakayofanyika Mkoani Simiyu kwa Kauli mbiu KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA BAADAYE