Home Mchanganyiko MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI VISHKWAMBI 700 KWA SHULE 10 ZA MSINGI ZA...

MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI VISHKWAMBI 700 KWA SHULE 10 ZA MSINGI ZA SERIKALI NA BINAFSI JIJINI DODOMA

0

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi,Akizungumza leo katika hafla ya ugawaji vishkwambi akimwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake za kuinua sekta ya elimu kwenye jimbo lake.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde,akizungumza na wadau wa Elimu pamoja na wanafunzi kutoka shule za msingi 10 ambapo amekabidhi Vishkwambi 700 kwa shule zilizopo Dodoma leo

Sehemu ya maboksi yenye Vishkwambi 700 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde,kwa shule 10 za shule ya msingi ambapo ametoa kwa ajili ya kuinua Elimu kwa wanafunzi wa shule hizo zilizopo jijini hapo.

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi kumi zilizopata mgawao wa Vishkwambi  700 zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde,kwa ajili ya kuinua Elimu kwa wanafunzi wa shule hizo zilizopo jijini hapo.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi pamoja na baadhi ya walimu na viongozi wakionyesha Vishkwambi   zilizotolewa na   Mhe. Mavunde,ambapo amegawa vishkwambi 700 kwa shule za msingi 10 zilizopo jijini hapo.

Wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa washikiria vishkwambi walipewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde ambapo amegawa Vishkwambi 700 kwa shule 10 za msingi zilizopo mkoani Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe Patrobas Katambi akimkabidhi cheti Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde alichopewa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Dodoma kutokana na mchango wake wa kusaidia Elimu ambapo leo amegawa vishkwambi 700 kwa shule 10 za msingi kwa ajili ya wanafunzi.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma  Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wanafunzi mara naada ya kugawa vishkwambi 700 kwa shule 10 za msingi kwa ajili ya wanafunzi.

………………………………………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Shule 10 za msingi za serikali na binafsi jijini Dodoma, zimepatiwa vishkwambi 700 ili kuongeza chachu ya wanafunzi kufanya vizuri kwenye masomo yao na kufundishwa kwa mfumo wa Tehama.
Vishkwambi hivyo vimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Anthony Mavunde ambaye ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu akishirikiana na taasisi ya Don Bosco na Shirika la Profuturo ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa ugawaji wa vishkwambi kwa wanafunzi ili wajifunze na kusoma kielektroniki.
Akizungumza leo katika hafla ya ugawaji vishkwambi akimwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi, amempongeza Mbunge huyo kwa jitihada zake za kuinua sekta ya elimu kwenye jimbo lake.
“Nakupongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kutatua changamoto za elimu, tangu nimekuja Dodoma kama Mkuu wa wilaya nimejifunza jambo kubwa kupitia wewe la kuwapenda wananchi wako na kuwakomboa kielimu,”amesema.
Katambi amezitaka shule zilizonufaika na msaada huo kuvitunza vifaa hivyo na kuvitumia kuchochea ufaulu kwa wanafunzi.
“Lazima Dodoma iwe tofauti na majiji mengine kiteknolojia na katika hili Mavunde umefanya kwa vitendo,”amesema.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi huyo, Mbunge Mavunde amelishukuru shirika la Profuturo kwa kuchangia sekta ya elimu na mkakati wa kulifanya jiji la Dodoma kama moja ya maeneo ya matumizi ya sayansi na teknolojia.
Amesema kutolewa kwa vishkwambi katika Shule ni awamu ya pili ya muendelezo wa kuimarisha ufundishaji kwa kutumia mfumo wa Tehama ambapo awali vilitolewa 5,000 kwa shule 10.
Amebainisha ndoto yake kila siku ni kuona Jiji la Dodoma linapiga hatua kubwa kwenye elimu kwa kuzalisha vijana wengi wanaofaulu vizuri kwani anaamini kupata kwao elimu bora ndio njia ya wao kufanikiwa kwenye maisha na kuwa msaada kwa Taifa.
“Tunamshukuru Rais Dk.John Magufuli ametupa elimu bila malipo lakini hiyo haimaanishi sisi wengine hatuna wajibu tena, ni jukumu letu kumsaidia Rais kufikia azma yake ya kutoa elimu yenye viwango bora kwa watoto wa kitanzania,” amesema Mavunde.
Mavunde amesema ataendelea kutoa vifaa hivyo kwa shule zingine katika awamu zijazo ili watoto wa Dodoma wapate uelewa wa matumizi ya teknolojia wakiwa bado wadogo.
Akitoa maelezo ya mradi,Mwakilishi wa shirika hilo na Don Bosco Net, Padri Peter Mutechura, amesema vishkwambi hivyo vinagharimu Sh.Milioni 700 na vinalenga kuwanufaisha wanafunzi hao kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia wakiwa katika umri mdogo.
“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na Mbunge Mavunde kutatua changamito za elimu jimbo la Dodoma mjini,”amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Dodoma, Katibu wa CWT Mkoa amemshukuru Mavunde kwa namna ambavyo amekua bega kwa bega na walimu katika kuwapatia motisha na kurahisisha ufundishaji.