KUTOKANA na uchafunzi wa Vyanzo vya maji,Afya za wananchi wapatao laki 1.78 wanaoshi katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na pembezoni mwa mji ziko hatarini kukumbwa na magonjwa mbalimbali.
Hayo yamebainika kwenye ziara ya awamu ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ya awamu ya pili ya iringa mpya.
Mkuu wa mkoa alipokuwa akipokea taarifa kutoka kwa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) moja ya changamoto iliyotajwa nipamoja na kazi ya kuosha magari inayofanywa na vijana katika chanzo cha maji Ndiuka.
Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) Girbelt Kayange akitoa taarifa ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo kwa mkuu mkoa alisema kuwa moja kati ya changamoto ambazo zinaikabiri mamlaka hiyo ni uharibifu wa chanzo hicho kutokana na shughuli za kiuchumi zinazofanywa unaweza sababisha madhara makubwa kiafya kwa binadamu kutokana na gari zinazooshwa baadhi ya gari kubeba mafuta na kemikali za viwandani.
“Kwa zaidi ya miaka 10 shughuli za kuosha magari katika chanzo cha maji ndiuka kimekuwa ni changamoto kubwa ambayo inaweza kuathiri afya za wananchi wanaotumia maji hayo” alisema
Aliongeza kuwa zipo taasisi za serikali ambazo zinakawamisha utendaji kazi wa mamalaka hiyo ikiwemo magereza jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za mamlaka hiyo kutokana na kudaiwa fedha nyingi za fedha.
‘’Bado tasisi za serikali hazijamaliza madeni yake licha ya baadhi ya kuliapa taratibu madeni hayo.lakini magereza wanadaiwa kiasi cha milioni 300.
Akitaja mafaniko ambayo mamlaka hiyo imeweza kupata nipamoja na kuongezeka kwa mapato,mamlaka imeweza kupanua mtandao wa maji safi na taka ukilinganisha na hapo awali na kusababisha kuwafikia wakazi wengi zaidi hasa wanaoishi pembezoni mwa Manispaa hiyo.
Akikagua mradi wa maji katika eneo la Ndiuka mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi alipiga marufuku shughuli za uzalishaji mali na za kibidamu kufanyika katika maeneo ya vyanzo vya maji na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuanza kuwachukulia hatua madereva ambao watabainika kusimamisha magari yao katika eneo la ndiuka kwa ajili ya kuoshwa na wakiwemo waoshaji.
Alisema gari nyingine zinabeba kemikali kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali viwandani pamoja na mafuta,kuendelea kuruhusu magari kuoshwa katika vyanzo vya maji ni kuatarisha usalama wa watu na afya zao.
‘’Napiga marufuku kuanzia leo shughuli za kuosha magari katika vyanzo vya maji pia naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwashukulia hatua stahiki madereva na wale wote watakaobainika kuosha magari kuanzia leo’’
Omary Mkangama Ofisa Utumishi Manispaa ya Iringa akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa alisema baada ya kupokea taarifa ya zuwio watatafuta eneo mbadala ambalo litatumika na vijanahao kufanya shughuli zao ambazo wamekuwa wakizifanya.
Alisema kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wanajishughilia na kazi ya kuosha magari katika eneo ambalo ni chanzo cha maji,jambo ambalo linatishia usalama wa afya wananchi wa mkoa wa Iringa.
Katika ziara hiyo alikagua miradi ya maji iliyo chini ya usimamizi wa IRUWASA katika eneo la Ndiuka ambalo ni chanzo cha maji, kukagua usambazaji wa maji katika eneo la Tosamaganga, mradi wa usambazaji wa maji kalenga ,kukagua mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji mtwivila pamoja na kuzungumza na kupokea kero wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Isakalilo.