Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI ARIDHISHWA NA KASI YA USAMBAZAJI UMEME KWENYE TAASISI ZA UMMA

NAIBU WAZIRI ARIDHISHWA NA KASI YA USAMBAZAJI UMEME KWENYE TAASISI ZA UMMA

0

Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu akiwa tayari amewasili kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya wa Liwale, alipokuwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme katika Wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi.

Naibu Waziri wa Nishati, akipata taarifa wa hali ya umeme ya Wilaya ya Liwale kutoka kwa Meneja Tanesco wa Wilaya ya Liwale Festo Nhembo wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme.

Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,akiongea na wananchi wa kata ya Liwale mjini kabla ya kuwasha umeme kwenye shule ya msingi ya kata hiyo, kulia Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Vicent Chiwambwa.

Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifurahi pamoja na kina mama wa kijiji cha Makata, mara baada ya kuwashwa kwa umeme kwenye zahanati ya kijiji hicho kilichopo kata ya Makata,Wilaya wa Liwale Mkoa wa Lindi.

Wananchi wa kijiji cha Makata wakimsikiliza Naibu waziri wa Nishati Subira Mgalu alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini humo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme kijijini humo.

*****************************

Hafsa Omar-LINDI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema amefurahishwa na kuridhishwa na kasi ya uunganishwaji umeme kwenye Taasisi za Umma zilizopo Wilayani Liwale kama Serikali ilivyoagiza.

Ameyasema hayo,Februari 24,2020,kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Liwale mjini na wa kijiji cha Makata, Kata ya Makata, Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi kabla ya kuwasha umeme kwenye Zahanati ya kijiji hicho na kwenye ya Shule ya Msingi Naluleo.

Aidha, alisema ziara yake hiyo,Mkoani humo lengo lake kukagua kazi za usambazaji umeme zinavyoendelea katika Mkoa huo na pia kujionea mwenyewe kasi ya usambazwaji wa umeme katika Taasisi za umma kama Serikali ilivyoagiza zipelekewe umeme na amefurahishwa kuona shule na zahanati nyingi za Wilaya hiyo zimeunganishwa na huduma hiyo.

“Rais Dkt.John Pombe Magufuli aliagiza umeme huu tunavyoupeleka vijijini basi tunganishe kwenye taasisi za umma hususani Shule,Zahanati, vituo vya afya,miradi ya maji, ofisi za Serikali kwahiyo nimefurahi leo tunazindua kwenye shule ya Msingi ambao Watoto wenu wanasoma hapa”Alisema.

Alisema, lengo la kupeleka umeme kwenye Taasisi hizo, kuhakikisha kuwa huduma hizo zinazotolewa zinakuwa za kiwango na zenye kukidhi mahitaji ya wananchi.

Alieleza kuwa, unganishwaji umeme katika kwenye Shule ya kijiji hicho utaongeza ufaulu wa wanafunzi katika shule hiyo,kwakuwa kutakuwa na kambi ya kujisome yenye uhakika wa usalama kwasababu mwanga utapatikana muda wote katika shule hiyo na wanafunzi kuweza kujisomea.

Vilevile, alisema kupatikana kwa umeme kwenye Zahanati kwenye kata ya Makata itasaidia kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwenye zahanati hiyo ambapo huduma hizo zinatolewa zitapatikana kwa muda wote na hakutakuwa na kisingizo cha kutotoa huduma kwasababu ya giza.

Pia, aliwataka wananchi wa vijiji hivyo wasitumie umeme kwa matumizi ya nyumbani, bali watumie umeme huo katika kujiletea maendeleo kwa kujiajiri kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato.

“ Tumieni umeme kujiletea maendeleo,kazi ya umeme ni pamoja na usalama majumbani,uboreshaji wa huduma za afya,umeme unasaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja, na kwa jamii kwa familia na Wilaya pia nataka Liwale iende mbali kiuchumi na nawalika wawekezaji wakubwa na wadogo waje kuwekeza kwasababu kuna umeme wa uhakika” Alisema.

Nae mbunge wa jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka ameishukuru Serikali kwa kufanya kazi kubwa ya usambazaji umeme nchini na kupeleke huduma hiyo kwenye wilaya humo na kuahidi kuwa wananchi wa jimbo hilo watautumia umeme kwa matumizi sahihi ambayo yatasaidia kujiletea maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kwa wilaya pia.